Imam Hussein(as)
-
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Kidini katika masuala ya Hija na Ziara:
"Kufuata mtindo wa maisha wa Imam Hussein (a.s) ni suluhisho kwa changamoto za jamii ya leo"
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Kidini katika Masuala ya Hija na Ziara, katika hafla ya kufunga tukio la pili la kimataifa la vyombo vya habari “Nahnu Abna’ Al-Husayn (a.s)”, alisisitiza umuhimu wa kunufaika na mtindo wa maisha na mafundisho ya Imam Husayn (a.s) ili kujibu mahitaji ya jamii ya leo.
-
Takriban Milioni 16 Washiriki Ziara ya “Jamandegan Arubaini” Iran
Ibara ya "Jamandegan Arubaini” inahusu wale walioshindwa kwenda ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as) katika Ardhi ya Karbala, lakini wanasherehekea tukio hilo kwa kufanya ibada na mikutano ya Maadhimisho ya Arubaini ya Imam (as) tokea mahali pale walipo.
-
Shukrani za Balozi wa Iran kwa Marjaa, Serikali na Wananchi wa Iraq kwa Kufanikisha Maadhimisho ya Arubaini
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq, Bw. Muhammad Kazim Al-Sadiq, ametuma tamko maalum la shukrani kwa Marjaa wa kidini, serikali, wananchi, hasa makabila, vijana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Iraq kwa kufanikisha maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s).
-
Huduma za Afya Bure kutoka Kituo cha Afya cha Razavi Mkoa wa Gilan katika Kituo cha "Waliobaki" wa Arubaini Rasiht
Katibu wa Kituo Maalumu cha Huduma za Afya cha Razavi Mkoa wa Gilan ametangaza juu ya utoaji wa huduma za bure za kitabibu na afya na kikundi cha kijitolea cha “Huduma na Upinzani wa Razavi” wakati wa hafla ya waliobaki wa Arubaini ya Imam Husain (a.s) katika Uwanja wa Manispaa ya Rasht.
-
Arubaini: Jukwaa la Haki, Amani na Uadilifu, na ni Taa ya Uongofu na Jahazi la Uokovu
Historia inaonyesha kuwa jukwaa hili lina mizizi imara katika imani, haki na uadilifu. Lilianza na mtu mmoja au wawili zaidi ya karne kumi zilizopita. Pamoja na changamoto nyingi zilizowakumba waliolipanda, idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila mwaka - hasa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
-
Wapenzi wa Imam Hussein (as) 36,000 wa Gilan Wajiandikisha kwa ajili ya Arubaini / Waanza Kurudi Nyumbani Taratibu
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Arubaini mkoa wa Gilan ametangaza kuanza kwa kurejea taratibu kwa mahujaji wa Arubaini mkoani humo na kusema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 36,000 kutoka Gilan wamejiandikisha kwenye mfumo wa Samah ili kushiriki katika maadhimisho ya kimataifa ya Arubaini ya Imam Husein (a.s).
-
Ubaguzi Dhidi ya Wafuasi wa Shia Nchini Punjab: Serikali Yatumia Shinikizo na Vitisho Kukomesha Maandamano ya Arbaeen Husseini (as)
Serikali ya Punjab imewaita wamiliki wa vibali vya kufanya maombolezo, waandaaji wa vituo vya kutoa huduma za bure (maisha ya Sadaka) na wajumbe wa kamati za ulinzi, na kuwashinikiza watangaze rasmi kujitenga na matembezi ya Arbaeen kuelekea Karbala.
-
Ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s.): Maana na Athari Zake
Ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s.) ni shule kamili ya roho, akili, jamii, na siasa. Ni fursa ya kuimarisha imani, kukuza undugu, kupandikiza roho ya kupinga dhulma, na kudumisha kumbukumbu ya kujitolea kwa ajili ya haki. Kuendeleza ibada hii ni njia ya kudumisha maadili ya kimungu na kibinadamu, na kuisambaza kwa vizazi vijavyo.
-
Kuzuiwa kwa njama ya ISIS ya kulenga Mazuwwari wa Arubaini / Magaidi 22 wakamatwa
Gavana wa Karbala ametangaza kufanikiwa kuzuia njama ya kigaidi iliyolenga kushambulia mahujaji wa Arubaini wa Imam Hussein (a.s).
-
Funzo Kuu la Arbaeen ni Msimamo Imara, Subira, na Mapambano: Ayatollah Ramazani
Mkutano wa awali wa wavuti (webinar) ulioandaliwa na Idara ya Masuala ya Kimataifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s.) kuhusu mada “Kutathmini Ujumbe wa Kimataifa wa Arbaeen ya Imam Hussain (a.s): Kutoka Wilayat hadi Wajibu” umefanyika.
-
Chanzo: Tovuti Rasmi ya Ofisi ya Ayatollah Makarim Shirazi | Je, Sheria ya Mtume (s.a.w.w) Inaruhusu Kuuawa kwa Imam Hussein (a.s)?
Kwa mujibu wa Aya ya "Tathira" (Qur’an, Ahzab: 33), Ahlul-Bayt (a.s), akiwemo Imam Hussein(as), wamesafishwa (wametakaswa) na Mwenyezi Mungu dhidi ya dhambi. Hivyo, haiwezekani Imam kuwa chanzo cha fitina au kuvunja umoja.
-
Chini ya Uangalizi wa Shirika la Habari la Abna:
Maelezo ya Tukio la Pili la Vyombo vya Habari “Nahnu Abna Al-Hussain (AS)” Yatangazwa / Formati, Tuzo, Njia za Kuwasilisha Kazi, na Picha ya Tangazo
Tukio la pili la vyombo vya habari “Nahnu Abna Al-Hussain (AS)” linakusudia kukuza na kuunga mkono kazi za kisanii na vyombo vya habari wakati wa msimu wa Arbaeen kwa mtazamo wa kimataifa, likionyesha uwepo wa mataifa mbalimbali, tamaduni, na dini, na litakubali kazi (Mawasilisho) kutoka kwa Mazuwwari wa Arbaeen.
-
Njia ya Karbala: Safari ya Kiroho Isiyoisha - Kila Hatua ni Mstari wa Mapenzi kwa Hussein (a.s)
Safari ya Arubaini katika Ardhi ya Karbala, inatengeneza Ukaribu wa Kiroho na Hussein (a.s) Katika Kila Hatua unayoipiga ukielekea kumzuru Aba Abdillah Al-Hussein (as).
-
Siku ya 11 baada ya A'shura | Karbala imetenganisha Kati ya Dini ya Kuabudu Matwaghuti (Bani Umaiyya) na Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu
Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) baada ya vita vya Karbala iliwakilishwa na damu ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbaka ambayo ilikuwa kielelezo hai cha dini ya haki ya Mwenyezi Mungu.
-
A'shura-Tanzania | Kuelimika Juu ya Tukio la A'shura na Tukio lolote la Historia ya Kiislam ni kusimamia Ukweli Halisi na Haki ilivyo Katika Historia
Tunasoma Matukio ya Historia ya Kiislamu ili Kuelimika na baada ya Kuelimika Tunasimama katika Msingi wa Haki na kusema ukweli Halisi wa Kihistoria ulivyo andikwa katika Vyanzo Sahihi vya Shia na Sunni.
-
Mimbari ya Imam Hussein (as) - Nchini Malawi | "Tofauti kati ya Mtu anayemjua Imam Hussein (AS) na Asiyemjua Imam Hussein (as)"
Sheikh Abdul Rahman Kachere: "Mtu anayemfahamu Imam Hussein (AS) daima ni jasiri katika kukabiliana na dhulma".Kumjua vizuri Imam Hussein (as) kutawafanya watu wa mataifa mbalimbali kumpinga adui na dhalimu, na kutambua njama za adui na dhalimu dhidi ya mataifa yao, na kuwa tayari kupambana kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwa ajili ya kuondoa uistikbari, dhulma na unyonyaji wa mfumo mpya wa ukoloni unaoitwa: Ukoloni mambo leo.
-
Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"
Vijana Waumini wa Kiislamu walicheza nafasi muhimu, yenye ufanisi mkubwa na athari chanya katika Vita vya Karbala. Karbala ilikuwa imejaa vijana, na mmoja wao alikuwa ni "Qasim bin Hassan". Alikuwa kijana na shujaa, na pia alikuwa anayo maanadalizi ya kutosha, kwa sababu alikuwa na moyo safi na wenye utimamu.
-
Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura | Kulinda Haki na Uhuru wa Watu ni Muhimu zaidi kuliko Maisha binafsi
Haki ya mtu binafsi na umma: Imam Hussein alijua kwamba alikuwa akielekea kifo, lakini alikusudia kuonyesha ulimwengu kuwa kulinda haki na uhuru wa watu ni muhimu kuliko maisha binafsi. Maombolezo ya Ashura yanatufundisha kuwa watu wanapaswa kuwa tayari kujitolea, si tu kwa ajili ya nafsi zao, bali kwa ajili ya ustawi wa jamii.
-
Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu
Imam Hussein (A.S) alikuwa ni mfano wa rehema ya Mwenyezi Mungu duniani. Mapambano na msimamo wake ni darasa kwa Umma. Kwa hiyo: 1_Waislamu waitikie wito wa Imam Hussein (A.S). 2_Waonyeshe huruma kwa wengine. 3_Watubu na wafanye toba kwa kupitia Ahlulbayt ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.
-
Rais wa Iran Dkt.Pezeshkian: "Tumejifunza kutoka kwa Hussein bin Ali (AS) namna ya Kutonyenyekea, Kutokuwa dhalili na kusujudia dhulma"
Rais wa Iran amesisitiza: Tumejifunza kutoka kwa Imam Hussein ibn Ali (AS) kutonyenyekea, kutojidhalilisha na kutosujudia dhulma.
-
Imam Baqir (a.s): Kutoka Machozi hadi Fikra
"Ninapokusoma jina lako, nakushukuru kwa ukubwa wa maarifa yako, na pia nakumbuka machozi yako ya utotoni huko Karbala...". Maisha ya Imam Muhammad Baqir (a.s) yamejazwa na mafundisho ya kina na nyakati za tafakari ambazo hazileti tu machozi kwa mioyo bali pia huamsha fikra na akili. Katika kipindi kigumu cha historia, alitumia hekima na maarifa kuleta mwanga mpya katika mafahimu za Dini.