Shirika la Habari ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s) -ABNA-: "Ee nyota ya tano ang’avu angani ya Uimam!" Machozi yetu juu ya Imam Baqir (a.s) na machozi yake juu ya Imam Hussein (as) huko Karbala, sio tu ishara ya maumivu na changamoto alizozipata kwa wakati wake, bali yanakuwa mbegu za kuamsha fikra na kujitambua katika mioyo yetu kama wafuasi wake. Machozi yetu tunapoomboleza shahahda yake na pia machozi yake yeye Mwenyewe alipokuwa katika uwanja wa Karbala, ni ushahidi wa imani thabiti kwa haki na juhudi zisizo na kikomo za kuamsha watu kupitia maarifa yake aliyoyatoa katika umma huu wa Babu yake Muhammad (saww). Kwa upande mwingine, fikra za Imam Baqir (a.s) ziliwezesha kuanzishwa kwa taaluma nyingi za kiislamu na kuongoza vizazi vingi kuelewa vyema dini, Mwenyezi Mungu, na uhalisia wa maisha. Kutoka katika tafsiri ya Qur’an hadi katika sheria na maadili, na hapana shaka kuwa fikra zake ni daraja thabiti la kuelewa dini na maisha.Kwa hivyo, Imam Baqir (a.s) ni mfano wa muunganiko wa hisia na maarifa; uso uliojaa upendo wa moyo na akili iliyo wazi na yenye harakati, aliweka nuru katika njia ya ukweli.
"Ee nyota ya tano ang’avu angani ya Uimam!"
Ee nyota ya tano inayong'aa angani katika uongozi wa Imamat (Uimam)!
Ee Baqir al-Ulum, wewe ambaye maarifa yalitangazwa kutoka kwenye kifua chako!
Jinsi gani mtu anaweza kukuambia wewe bila kutaja maumivu ya Karbala?
Wewe ulikuwa mtoto na shuhuda wa maafa makubwa, ambayo anga ililia duniani na jua likafunikwa na giza.
Katika jangwa kali la moto la Karbala, katikati ya kiu na damu, macho yako madogo, yaliona tukio lililoshika mioyo ya watu milele kwa huzuni.
Uliwaona jinsi walivyovuka mipaka juu ya miili ya wapendwa wako, uliwaona jinsi walivyomimina mishale na visu juu ya Mwili Mtukufu wa Hussein (a.s)...
Lakini wewe, Imam Baqir (a.s), kutoka kwenye majivu ya moto ya Karbala, uliotesha mti wa maarifa na hekima. Maarifa yako yalibeba sauti ya Ashura moyoni, na mafundisho yako, yakawa kioo cha kujitolea na shahada.
Leo, ninapokusoma jina lako, nakupongeza kwa ukubwa wa maarifa yako, na pia nakumbuka machozi yako ya utotoni Karbala...
Ulimfundisha mtu kuwa hata kutoka giza la usiku, mwezi wa mwanga wa kuongoza unaweza kuangaza.
Salamu kwako, Ee Baqir al-Ulum!
Salamu kwako, Ee mtoto aliyeachwa na maumivu ya Karbala!
Salamu kwako, Ee ambaye daima umehifadhi kumbukumbu na jina la Ashura hai!
Imeandikwa na: Fatemeh Pourabbas.
Your Comment