Ninawapa pole familia za mashahidi hawa wapendwa na wananchi wote wa Yemen.
Tunawakumbuka mashahidi wote wa Uislamu: kuanzia mashahidi wa tukio la Fakh, mashahidi wa Palestina, Lebanon, na mashahidi wetu wa Iran kama vile Shahidi Qassem Soleimani na wengine.
"Ninapokusoma jina lako, nakushukuru kwa ukubwa wa maarifa yako, na pia nakumbuka machozi yako ya utotoni huko Karbala...".
Maisha ya Imam Muhammad Baqir (a.s) yamejazwa na mafundisho ya kina na nyakati za tafakari ambazo hazileti tu machozi kwa mioyo bali pia huamsha fikra na akili. Katika kipindi kigumu cha historia, alitumia hekima na maarifa kuleta mwanga mpya katika mafahimu za Dini.