28 Juni 2025 - 17:21
Rais wa Iran Dkt.Pezeshkian: "Tumejifunza kutoka kwa Hussein bin Ali (AS) namna ya Kutonyenyekea, Kutokuwa dhalili na kusujudia dhulma"

Rais wa Iran amesisitiza: Tumejifunza kutoka kwa Imam Hussein ibn Ali (AS) kutonyenyekea, kutojidhalilisha na kutosujudia dhulma.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Dakta Masoud Pezeshskian, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alihudhuria hafla ya maziko ya makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nchi ya Iran waliouawa shahidi kufuatia uchokozi wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na makundi mbalimbali ya umma, Jumamosi hii asubuhi (78-06-2025), kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa mashahidi hao.

Rais pia alitweet: "Ninawashukuru, wananchi wapendwa, kutoka chini ya moyo wangu; mliojitokeza kushiriki katika mazishi na maziko ya mashahidi wa nchi kwa upendo, na sauti ya umoja wetu imeyafikia masikio ya ulimwengu.

Tumejifunza kutoka kwa Hussein ibn Ali (AS) kutonyenyekea na kutosujudia dhulma. Kutumikia Taifa huru kama hili ni heshima ya maisha yangu. Iran Daima."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha