dhulma
-
Mimbari ya Imam Hussein (as) - Nchini Malawi | "Tofauti kati ya Mtu anayemjua Imam Hussein (AS) na Asiyemjua Imam Hussein (as)"
Sheikh Abdul Rahman Kachere: "Mtu anayemfahamu Imam Hussein (AS) daima ni jasiri katika kukabiliana na dhulma".Kumjua vizuri Imam Hussein (as) kutawafanya watu wa mataifa mbalimbali kumpinga adui na dhalimu, na kutambua njama za adui na dhalimu dhidi ya mataifa yao, na kuwa tayari kupambana kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwa ajili ya kuondoa uistikbari, dhulma na unyonyaji wa mfumo mpya wa ukoloni unaoitwa: Ukoloni mambo leo.
-
Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura | Kulinda Haki na Uhuru wa Watu ni Muhimu zaidi kuliko Maisha binafsi
Haki ya mtu binafsi na umma: Imam Hussein alijua kwamba alikuwa akielekea kifo, lakini alikusudia kuonyesha ulimwengu kuwa kulinda haki na uhuru wa watu ni muhimu kuliko maisha binafsi. Maombolezo ya Ashura yanatufundisha kuwa watu wanapaswa kuwa tayari kujitolea, si tu kwa ajili ya nafsi zao, bali kwa ajili ya ustawi wa jamii.
-
Rais wa Iran Dkt.Pezeshkian: "Tumejifunza kutoka kwa Hussein bin Ali (AS) namna ya Kutonyenyekea, Kutokuwa dhalili na kusujudia dhulma"
Rais wa Iran amesisitiza: Tumejifunza kutoka kwa Imam Hussein ibn Ali (AS) kutonyenyekea, kutojidhalilisha na kutosujudia dhulma.
-
Maana ya Maneno ya Ayatullah Ustadh Abdullah Jawadi Amuli kwamba: “Rudisha jiwe, kule lilipotoka”
Katika uwanja wa kisiasa, kauli hii inaweza kumaanisha kuwa taifa au jamii halipaswi kuruhusu kushambuliwa, kupuuzwa au kudhulumiwa na adui wa ndani au wa nje, bali lazima ichukue hatua za kulinda maslahi yake kwa ujasiri.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji: "Ulimwengu wa Kiislamu wahitaji kutekeleza mafundisho ya Hija ili kusitisha maafa ya Gaza"
Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu kwa sasa unayahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote mafundisho ya Hija, na akibainisha kuwa Hija ya mwaka huu ni msimu wa pili unaofanyika sambamba na jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza, ameuliza swali lifuatalo:“Ni nani anapaswa kusimama dhidi ya janga hili la kibinadamu?” Kisha ameongeza kwa kusisitiza: “Bila shaka yoyote, serikali za Kiislamu ndizo zinazobeba wajibu wa kwanza wa jukumu hili, na mataifa ya Kiislamu yana haki ya kudai utekelezaji wa wajibu huo kutoka kwa serikali zao.”
-
Palestina lazima ibaki / Watawala wetu wamepotoka kutoka kwenye Misingi ya Umma wa Kiislamu
Mwenyekiti wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiunga mkono Palestina amesema kuwa, watawala na wanasiasa wa sasa wa nchi hiyo wamejitenga na thamani halisi za Umma wa Kiislamu.