Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maana ya Maneno ya Ayatullah Ustadh Abdullah Jawadi Amuli kwamba: “Rudisha jiwe, kule lilipotoka.” Maneno haya, yana maana pana na ya kina katika uwanja wa maadili, siasa na maisha ya kila siku. Ifuatayo ni sehemu ya ufafanuzi wa kina juu ya maneno hayo:
Tafsiri na Maana ya Kauli Hii: “Rudisha jiwe, kule lilipotoka”
Kutokukubali dhulma au uonevu kwa kunyamaza. Ikiwa mtu au kikundi kitakutupia "jiwe" – yaani, kikufanyie uadui, madhara au kukuvunjia heshima – basi usikae kimya wala kuzembea. Inamaanisha kupambana na dhulma kwa hekima na msimamo.
Kulinda heshima na utukufu wa mtu binafsi na jamii
Kauli hii inahimiza mtu kutokubali kudharauliwa, hata kama madhara yametoka kwa mtu wa karibu au mgeni. Rudisha heshima yako kwa adabu lakini kwa msimamo.
Kwenye siasa na jamii:
Katika uwanja wa kisiasa, kauli hii inaweza kumaanisha kuwa taifa au jamii halipaswi kuruhusu kushambuliwa, kupuuzwa au kudhulumiwa na adui wa ndani au wa nje, bali lazima ichukue hatua za kulinda maslahi yake kwa ujasiri.
Kwa mantiki hiyo:
Kauli ya Ayatullah Jawadi Amuli ni mwongozo wa kimaadili na kistratejia unaohimiza:
1-Ujasiri dhidi ya dhulma.
2-Kulinda heshima binafsi na ya jamii.
3-Kutoa jibu sahihi kwa uovu kwa njia ya haki na busara.
Ni kauli inayofundisha kwamba:
“Uislamu si dini ya unyonge au kusamehe bila mipaka, bali ni dini ya heshima, ujasiri na haki.”
Your Comment