Tangu wakati huo ambapo Shetani aliasi na kukataa kumsujudia Adam (a.s), mzozo wa kihistoria kati yake na Mwanadamu ulianza; mzozo ambao unaendelea hadi leo hii. Lakini swali muhimu ni hili: Kwa nini Mwenyezi Mungu alimpa adui huyu katili (Shetani) muda mrefu wa kuendelea kuishi na kujaribu na kuwapoteza watoto wa Adam (Wanadamu)?!. Nakuletea Hadithi nzuri na yenye mazingitio ndani yake kuhusu Shetani na Mwanadamu, na utaijua sababu na siri ya Ruhusa ya Mwenyezi Mungu kwa Shetani ili aendelee kuishi kwa muda mrefu.
Imam Ali (a.s), Maisha yake yote yalikuwa ni Maisha ya kuweka uthabiti na kuimarisha nguzo na misingi ya Uislamu, pia kujitolea muhanga kwa kitu ghali na chenye thamani kubwa, ili kuhakikisha neno la Mwenyezi Mungu linakuwa juu, na neno la makafiri linakuwa chini.