Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana, tarehe 3 Dey, kundi la ISIS Khorasan baada ya kushindwa kuteka maeneo ya mashariki mwa Afghanistan katika miaka iliyopita, limebadilisha mkakati wake kutoka mapigano ya wazi ya kivita kwenda katika operesheni za mijini.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa ISIS katika miezi ya hivi karibuni imeanzisha nyumba za siri za makundi yake katika miji kama Kabul na Mazar-e Sharif, na hivyo kuhamishia wigo wa shughuli zake katika vituo vya miji.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa kundi hilo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita limefanya takribani mashambulizi 300 nchini Afghanistan, yaliyopelekea vifo vya angalau watu 800. Idadi ya wanachama wa ISIS Khorasan inakadiriwa kuwa takribani watu elfu mbili, na kwa mujibu wa taasisi hiyo, kundi hilo linaendelea kukua kwa kasi na kwa upana mkubwa, hususan katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Afghanistan.
Wakati huohuo, nchi ya Pakistan imetangaza kukamatwa kwa Sultan Aziz Azzam, msemaji wa ISIS Khorasan. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wameonya kuhusu athari za kikanda za harakati za ISIS na nafasi ya wahusika wa kikanda katika muktadha huo.
Your Comment