Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Saeed Ziad, mtangazaji maarufu katika Televisheni ya Al Jazeera amesema: "Ikiwa uchokozi wa Marekani haungejibiwa na Iran, basi Marekani ingeenda mbele zaidi na kuingilia kirahisi vita kati ya Iran na Israel. Aliendelea kubainisha hali ya mambo ilivyo kuwa" "Licha ya juhudi zote za kuishawishi Iran isifanye hatua yoyote ya majibu yake ya mashambulizi kwa Marekani na badala yake iishie tu kuhusika katika mashambulizi dhidi ya Israel pekee, Iran iliamua kupanua wigo wa majibu yake ya mashambulizi ya makombora, na kwa mara ya kwanza, Iran ikavishambulia kwa Makombora vituo vya Kijeshi vya Marekani vilivyopo katika Mashariki ya Kati.
Ujasiri huu wa Iran ulikuwa wa kuzuia hamu ya Marekani ya kutaka kuingilia kati vita vya israel dhidi ya Iran - ili kuisaidia na kuiokoa Israel (iliyokuwa imelemewa na vita)- . Na Ikiwa uchokozi huu haungejibiwa na Iran, Marekani ingejiona kuwa shupavu zaidi na kuiona Iran dhaifu au kwamba inaogopa na hatimae wangeenda mbele zaidi na kuingilia vita (ya Israel aliyoianzisha dhidi ya Iran kupitia mahesabu mabaya yaliyoigharimu na kuifanya israel igeuzwe kuwa magofu).
Your Comment