Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maombolezo ya A'shura Nchini Tanzania yamefanyika kwa mafanikio makubwa katika mwaka wa Maombolezo ya Muharram 1447 Hijria. Viongozi mbalimbali wa Taasisi mbalimbali za Kiislamu na Kiserikali wamehudhuria katika Maandamano haya ya Amani yaliyofanyika katika Mutaa ya Posta Jijini Dar-es-salaam - Tanzania. Viongozi hao ni pamoja Hojjat al-Islam wal-Muslimin, Dr. Ali Taqavi - Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Tanzania. Wengine ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu na Viongozi wengine wa Kiserikali na Kiroho.
Baada ya vikao vya Maombolezi ndani ya kumbi za Hussainiyya, sasa Mwezi kumi mfungo tatu matembezi yamefuatia. Waumini Wafuasi na Wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) kote Duniani, Leo hii wametoa nje na kufanya Masira ya Amani barabarani na kupaza sauti zao sauti za Maombolezo ya Mauaji ya Karbala dhidi ya Mjukuu wa Mtume (saww).
Kihistoria: Mwaka wa 61 Hijria, kulitokea tukio ambalo vitabu vya historia vimelisimulia, ni tukio la kuuwawa kikatili Mjukuu huyo wa Mtume (saww), Al-Imam Al-Hussein (a.s) na Masahaba wake.
Sio kwamba waovu walimuua kinyama kwa kuwa alikuwa na kosa, la hasha! Bali Hlhakuwa na kosa lolote, ni kwa sababu tu alikataa kumpa kiapo cha utii mtu muovu, aliye jipachika kwenye Nafasi ya utawala wa Umma wa Kiislamu, aliyesifika kwa Sifa chafu za ulevi, kucheza na Wanawake hadharani, mauaji, na kila aina ya sifa mbaya, naye si mwingine Bali ni muovu Yazid bin Muawia (L.A).
Wanahistoria waliandika haya na Mengi zaidi ili watu wasome na waelimike, na waijue Haki na batili na kujitenga na batili.
Unapoona Waislamu wanakaa na Kuzungumzia Tukio la A'shura na kulaani Mauaji ya Yazid bin Muawia.... ujue kuwa wamesema Matukio yote ya kihistoria yaliyopo katika vitabu vya Kisunni na kishia juu ya Tukio la Karbala... na wamesoma kisha wakaelimika na sasa wanasimama katika nafasi ya kusema Haki na ukweli juu ya Historia sahihi na ya Haki iliyo andikwa juu ya Tukio la A'shura na Mapinduzi ya Kiislamu ya Imam Hussein (as).
Your Comment