Mbinu za vyombo vya habari katika kueneza batili na kuunda shubha ili kuwazamisha watu ndani ya fikra zisizo za Kimungu zimekuwa zikitumiwa na wapinzani wa njia ya haki katika vipindi vyote vya historia. Ingawa njia hizi hubadilika kulingana na zama, malengo yao hubaki yale yale.
Kurejea mbinu hizi katika mojawapo ya barua za Imam Ali (a.s) kwa Muawiya na kulinganisha na mbinu za vyombo vya habari vya kigeni katika ulimwengu wa leo kunadhihirisha ukweli kwamba “Muawiya na wanaofanana naye” katika historia wamejitahidi kupotosha wengine ili kufikia malengo yao wenyewe-juhudi ambazo hatimaye hupelekea maangamizi yao pamoja na maangamizi ya wale wanaowafuata.
Tunasoma Matukio ya Historia ya Kiislamu ili Kuelimika na baada ya Kuelimika Tunasimama katika Msingi wa Haki na kusema ukweli Halisi wa Kihistoria ulivyo andikwa katika Vyanzo Sahihi vya Shia na Sunni.