30 Juni 2025 - 20:21
Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Vijana Waumini wa Kiislamu walicheza nafasi muhimu, yenye ufanisi mkubwa na athari chanya katika Vita vya Karbala. Karbala ilikuwa imejaa vijana, na mmoja wao alikuwa ni "Qasim bin Hassan". Alikuwa kijana na shujaa, na pia alikuwa anayo maanadalizi ya kutosha, kwa sababu alikuwa na moyo safi na wenye utimamu. 

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, tarehe (30 - 06- 2025), Majalisi za Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as) zimeendelea katika Madrasa ya Mabinti wa Kiislamu inaypitwa Madrasat Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-Salaam Tanzania. Khatibu wa katika Majlisi hii, alikuwa ni: Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin, ambaye aliwasilisha mada muhimu iliyohusiana na: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala".

Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Katika ardhi ya Karbala, Kijana Shujaa, Qasim bin Hassan bin Ali (as) alimuomba idhni Imam Hussein (as) aili aweze kuingia katika uwanja wa mapambani dhidi ya maadui wa Uislamu.

Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Imam Hussein (as) alimruhusu Qasim bin Hassan (as), ambaye alikuwa Kijana shujaa, na akaingia uwanjani na kupambana kishujaa kwa ajili ya Uislamu

Qasim (as), alikuwa kijana na shujaa, na pia alikuwa anayo maanadalizi ya kutosha na utayari wa kuihami Dini yake Tukufu ya Kiislamu, kwa sababu alikuwa na moyo safi na wenye utimamu

Katika mada hii, Khatibu alijadili mengi sambamba na wanafunzi kuhusiana na dauru au jukumu muhimu la vijana katika vita vya Karbala, na zifuatazo ni nukta muhimu alizozitolea ufafanuzi kwa kina: (1) Ujana katika Uislamu (2) Qasim bin Hassan.

Kuhusiana na nukta ya ujana, Khatibu alibainisha kwamba kuna mambo kadhaa ambayo Wanadamu hawayapi umuhimu wala kuyathamini:

Jambo la Kwanza ni: Ujana

 Katika umri wa ujana, kijana anakuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi mazuri na yenye athari chanya katika jamii, lakini kama kijana hughafilika na ujana wake na kutouthamini mpaka wakati ule anapokuwa katika Umri wa Uzee na kuwa katika hali ya kutokuwa na ule uwezo wa ujanani, hapo ndipo anapojuta na kukumbuka thamani ya ujana, na kwa wakati huo ujana haurudi.

Jambo la pili ni: Afya

Mwanadamu kawaida hughafilika na mpaka katika suala la afya, kiasi kwamba huwa hahisi thamani ya afya yake, mpaka anapokuwa mgonjwa na dhaifu, hapo ndipo huitambua thamani ya afya ya mwili wake.

Siku moja Imamu Sadiq (AS) alimtuma mmoja wa Wanafunzi wake kwenda sehemu kufanya Tabligh (Kuhubiri). Aliporudi, Imam Sadiq (AS) alimuuliza: "Umeonaje hali ya huko?". Mwanafunzi akajibu kwamba: "Nimeona watu wote walikuwa bize na shughuli (kazi) zao, na Dunia yao". Imamu Sadiq (AS) akasema: "Nyinyi mmesahau ujana (vijana), na mnapaswa kufanya kazi na vijana (ujana), lakini inaonyesha kuwa mnafanya kazi na wazee (uzee), sasa fanya kazi na vijana (ujana), kwa sababu vijana wana mioyo timamu na safi".

Vijana ni kama ardhi ambayo haijapandwa (kitu chochote). Vijana wana uwezo na nguvu sana. Na kwa sababu ujana ni hatua muhimu zaidi, basi na maandalizi ni muhimu pia. Na Harakati ya Mapinduzi ya Karbala ilikuwa imejaa vijana, na mmoja wao alikuwa ni "Qasim bin Hassan". Alikuwa kijana na shujaa, na pia alikuwa anayo maanadalizi ya kutosha, kwa sababu alikuwa na moyo safi na wenye utimamu. 

Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Ushujaa wa Kijana Qasim bin Hassan bin Ali (as) Katika Kujitolea na Kuutetea Uislamu, katika Uwanja wa Mapambano wa Karbala, ni somo kubwa na muhimu kwa Vijana wa Kiislamu

Mwisho: Tunakumbusha kama tulivyodokeza hapo juu, kwamba Majlisi hii ya Maombolezo ya Muharram na kuhuisha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Karbala, imefanyika katika Madrasat ya Mabanati (Wasichana) wa Kiislamu: Madrasat Harzat Zainab (sa) - Iliyopo Kigamboni, Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.

Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Nafasi ya Vijana Katika Mapinduzi ya Imam Hussein(as) Katika Ardhi ya Karbala"

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha