Shule ya Wasichana Hazrat Zainab (s.a.) iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, imeandaa darasa la Tafsiri ya Qur’ani Tukufu pamoja na maombolezo ya Imam Hussein (a.s.), ambapo washiriki walijadili athari za vita vya kisaikolojia katika kudhoofisha fikra, imani na maadili ya vijana.

27 Julai 2026 - 16:58

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Shule ya Wasichana Hazrat Zainab (s.a.) ya Kigamboni, Dar es Salaam, Tanzania, imeandaa darasa la Tafsiri ya Qur’ani Tukufu na hafla ya maombolezo ya Imam Hussein (a.s.), iliyohudhuriwa na wanafunzi 144 pamoja na msimamizi wa bweni.
 
Katika darasa hilo, lililoendeshwa na Ustadhah Fatimah Masumah Ali Dina, mjadala ulijikita katika suala la vita vya kisaikolojia na athari zake kwa vijana, hususan katika kuathiri fikra, imani na misingi ya kiroho.
 
Ustadhah huyo alieleza kuwa miongoni mwa malengo ya vita vya kisaikolojia ni kuwafanya vijana waathiriwe kimawazo na kiutamaduni, hatua ambayo inaweza kusababisha kudhoofika kwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu na kuwapeleka mbali na maadili na misingi ya kidini.
 
Aidha, ilielezwa kuwa zana mbalimbali za kisasa, zikiwemo simu za mkononi, mitandao ya kijamii, tovuti na michezo ya kidijitali, zinaweza kutumiwa kama njia za kuathiri fikra na mitazamo ya vijana. Kwa hiyo, vijana wametakiwa kuwa na uelewa, umakini na ulinzi wa imani na misingi yao ya kiroho.
 
Baada ya darasa hilo, washiriki walifanya maombolezo ya Imam Hussein (a.s.), wakikumbuka msimamo wake wa kujitolea kwa ajili ya haki, kupinga batili na kulinda maadili ya Mwenyezi Mungu.
 
Shughuli hiyo iliandaliwa na Shule ya Wasichana Hazrat Zainab (s.a), iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, Tanzania.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha