28 Julai 2026 - 14:10
Ufichuzi wa Kushtua wa Uhalifu Dhidi ya Watoto Wachanga wa Gaza

Aliyekuwa mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani amedai kuwa watoto wachanga 300 walipatikana katika makaburi ya muda ndani ya Ukanda wa Gaza wakiwa wamefungwa mikono nyuma, huku akidai walizikwa wakiwa hai. Amesema madai hayo hayajapata nafasi katika vyombo vikuu vya habari vya Marekani wala kujadiliwa na Bunge la nchi hiyo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Aliyekuwa mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani ametoa madai ya kutisha akisema kuwa watoto wachanga 300 walipatikana katika makaburi ya muda ndani ya Ukanda wa Gaza wakiwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo yao, huku akidai walizikwa wakiwa hai.

Kwa mujibu wa ushuhuda wake, jambo hilo halijapewa nafasi katika magazeti makubwa ya Marekani, wala halijawasilishwa kwa mjadala ndani ya Bunge la Marekani, hali ambayo amesema inaibua maswali makubwa kuhusu namna vyombo vya habari na taasisi za kisiasa zinavyoshughulikia taarifa zinazohusu maafa ya kibinadamu yanayoendelea Gaza.

Kauli hiyo imezua mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, ambapo wengi wameeleza kushtushwa na madai hayo na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa, huru na wa uwazi ili kubaini ukweli wa kilichotokea na kuhakikisha wahusika wowote wa uhalifu dhidi ya raia wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Madai hayo yanaendelea kusambaa huku yakisubiri kuthibitishwa na uchunguzi wa taasisi huru za kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha