26 Julai 2026 - 16:07
BEF Yaendeleza Wito wa Uchangiaji Damu Kwa Ajili ya Kuokoa Maisha ya Wengi

BEF imewahimiza wananchi kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika Jumapili, tarehe 2 Agosti 2026, katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala, ikisisitiza kuwa tone moja la damu linaweza kuwa chanzo cha uhai na tumaini kwa mtu mwingine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA -, Taasisi ya BEF imewahimiza wananchi kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa na wahitaji wa damu katika jamii.

BEF imesema kuwa kutoa damu ni miongoni mwa matendo ya kishujaa, kwa kuwa mchango wa damu unaweza kutoa tumaini kwa mtu anayehitaji msaada wa haraka na kuokoa maisha ya watu wengi.

Katika wito wake kwa wananchi, BEF imesisitiza kauli mbiu inayosema: “Ushujaa ni pamoja na kutoa tumaini pale linapohitajika.”
Aidha, BEF imewahimiza wananchi kuwa mashujaa kwa kuungana na timu hiyo katika zoezi la uchangiaji damu, ikieleza kuwa tone moja la damu linaweza kuwa uhai kwa mwingine.

Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika Jumapili, tarehe 2 Agosti 2026, katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala, kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo la kibinadamu, ambalo linaweza kusaidia kuongeza akiba ya damu na kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma za dharura na matibabu mbalimbali.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu zoezi hilo, wananchi wanaweza kuwasiliana na waandaaji kupitia namba ya simu: 0654 734 022.

BEF Yaendeleza Wito wa Uchangiaji Damu Kwa Ajili ya Kuokoa Maisha ya Wengi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha