Aliyekuwa mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani amedai kuwa watoto wachanga 300 walipatikana katika makaburi ya muda ndani ya Ukanda wa Gaza wakiwa wamefungwa mikono nyuma, huku akidai walizikwa wakiwa hai. Amesema madai hayo hayajapata nafasi katika vyombo vikuu vya habari vya Marekani wala kujadiliwa na Bunge la nchi hiyo.
Ripoti ya gazeti la The New York Times inafichua jinsi Jeffrey Epstein alivyokuwa na mtandao mkubwa wa wanasiasa, wafanyabiashara, na watu mashuhuri waliokuwa wakiufaidi ushawishi wake bila uwajibikaji. Licha ya ufichuzi huu mkubwa, hakuna mmoja kati ya watu hawa aliyehukumiwa, jambo linaloongeza kutoaminiana kwa umma na kuibua uvumi kuhusu vifo vya Epstein gerezani mwaka 2019.