28 Julai 2026 - 13:42
Ayatollah Jawadi Amoli: Iran haijawahi kuwa ya kwanza kushambulia na haitampa mvamizi usalama

Kiongozi wa kidini Ayatollah Abdullah Jawadi Amoli amesisitiza kuwa wananchi wa Iran hawajawahi kuwa wa kwanza kuanzisha mashambulizi dhidi ya wengine, na kwamba hawatampa usalama wala nafasi yoyote mvamizi yeyote, akisisitiza umuhimu wa kulinda usalama, utulivu wa nchi na umoja wa kitaifa.

Ayatollah Jawadi Amoli alitoa kauli hiyo katika hafla ya kuwakumbuka mashahidi 398 wa Jeshi la Iran iliyofanyika katika mji wa Amol, mkoani Mazandaran kaskazini mwa Iran, ambapo alieleza kuwa taifa la Iran limejengwa juu ya misingi ya ulinzi, uadilifu na kujilinda dhidi ya uonevu, si uanzishaji wa vita au uadui dhidi ya wengine.

Amesema wazi kuwa “taifa la Iran halijawahi kuwa chanzo cha uvamizi dhidi ya mataifa mengine, na halitompa nafasi wala usalama yeyote atakayelenga kuhatarisha amani na usalama wa nchi.”

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kudumisha umoja wa kitaifa na mshikamano wa wananchi katika kulinda misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na usalama wa nchi, akibainisha kuwa nguvu ya taifa ipo katika mshikamano wake.

Akizungumzia uhusiano wa kiroho wa wananchi wa Iran, Ayatullah Jawadi Amoli alibainisha kuwa jamii ya Iran imejikita katika utamaduni wa Ashura, akisema: “Taifa letu ni la Husseini, na roho ile ile iliyodhihirika katika harakati ya Imam Hussein (a.s) bado iko hai na inawaka katika nyoyo za watu wa ardhi hii.”

Pia aligusia ushiriki mkubwa wa wananchi katika nyanja za ulinzi wa nchi, akieleza kuwa uwepo wao na kujitolea kwao katika nyakati za ulinzi wa Mapinduzi na taifa ni ishara ya msaada wa Mwenyezi Mungu, na kwamba Mungu huwaandaa waumini kwa ajili ya kulinda dini yake na misingi yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha