Kulinda
-
Jukumu la Marajii wa Kidini wa Kishia katika;
"Kulinda Umoja wa Kitaifa na Utambulisho wa Iran / Sehemu ya Saba: Kisa cha Kuokolewa kwa Lugha ya Taifa ya Iran na Ukombozi wa Azarbaijan"
Kulinda umoja wa ardhi na kuzingatia utambulisho wa kidini ni miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakipewa umuhimu mkubwa na viongozi wa kidini katika ardhi za Kiislamu. Kiasi kwamba kila aina ya uvamizi au shambulio dhidi ya ardhi za Kiislamu ilikabiliwa na mwitikio mkali kutoka kwao. Uvamiuzi wa Azarbaijan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na juhudi za kuutenga mkoa huo kutoka Iran ni miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha tena ushawishi wa uongozi wa kidini katika kulinda umoja wa ardhi ya nchi. Aidha, kulinda utambulisho wa kitaifa wa Kiairani pia lilikuwa ni mojawapo ya masuala yaliyopatiwa umuhimu maalum na viongozi (Marajii) wa kidini katika kipindi cha utawala wa Pahlavi.
-
Kulaaniwa Vikali Shambulio Dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa India katika Mkutano wa Maandamano Mjini Lucknow
Hujjatul-Islam Muhammad Miyan Abidi Qummi: "Lengo kuu la mashambulio kama haya,” alisema, “ni kudhoofisha harakati ya ulinzi wa wakfu na kunyamazisha sauti ya wanaotetea haki.”
-
Nafasi ya Marājiʿ wa Kishia katika Kulinda Umoja wa Ardhi na Utambulisho wa Kitaifa- Sehemu ya 2 | Marāji ni, Walinzi wa Uhuru wa Nchi za Kiislamu
Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.