14 Oktoba 2025 - 09:04
Nafasi ya Marājiʿ wa Kishia katika Kulinda Umoja wa Ardhi na Utambulisho wa Kitaifa- Sehemu ya 2 | Marāji ni, Walinzi wa Uhuru wa Nchi za Kiislamu

Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt(as) -ABNA- Miongoni mwa majukumu muhimu ambayo Marājii wa Kishia wameyatekeleza kwa hekima na ujasiri ni kulinda uhuru na kujitawala kwa nchi za Kiislamu. Katika vipindi mbalimbali vya kihistoria, Marājiʿ hawa wamekuwa ngome madhubuti mbele ya uvamizi wa kigeni na juhudi za kikoloni zilizolenga kudhoofisha ulimwengu wa Kiislamu.

Kupitia fatwa, miongozo ya kijamii, na harakati za kisiasa zenye busara, Marājiʿ wa Kishia wamehimiza umoja wa Waislamu, kupinga ukoloni na kulinda heshima ya ardhi za Kiislamu. Wameona kuwa uhuru wa nchi na umoja wa ardhi ni sehemu ya imani na wajibu wa kidini, kwani ardhi ya Waislamu ni amana kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo lazima ilindwe kwa damu na nafsi.

Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.

Kwa mtazamo wa Kishia, heshima ya ardhi ya Kiislamu ni sawa na heshima ya dini na Waislamu. Hivyo, kulinda mipaka ya Kiislamu si jambo la kisiasa pekee bali ni jukumu la kisheria na kimaadili.

Marājiʿ hawa wamethibitisha kwamba uhuru wa kweli hautokani na silaha pekee, bali unatokana na uongozi wa kiroho, elimu, na mshikamano wa kidini na kitaifa.

Kwa njia hii, Marājiʿ wa Kishia wamekuwa walinzi wa uhuru wa nchi za Kiislamu na wahifadhi wa utambulisho wa Kiislamu, wakiwaunganisha wananchi chini ya bendera ya haki, maadili, na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha