Ayatullah
-
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan:
Uislamu ni mtangulizi wa haki sawa, uadilifu wa kiuchumi na utawala wa haki
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan amesema kuwa: Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ambao ni mtangulizi wa haki sawa, uadilifu wa kiuchumi na utawala wa haki, na mfano bora zaidi wa hayo ni mfumo wa haki wa Imam Ali (a.s) ambao utabaki kuwa kielelezo cha uadilifu na usawa daima.
-
Nafasi ya Marājiʿ wa Kishia katika Kulinda Umoja wa Ardhi na Utambulisho wa Kitaifa- Sehemu ya 2 | Marāji ni, Walinzi wa Uhuru wa Nchi za Kiislamu
Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.
-
Ayatullah Malakooti:
"ABNA Ina Wajibu wa Kutambulisha Madhehebu ya Ahlul-Bayt (A.S) Ulimwenguni / Baba Marehemu alikuwa wa Awali Kusaini kuondolewa kwa Shah"
Akizungumza na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (ABNA) Jumapili, 20 Mehr 1404 (2025), Ayatullah Malakooti alisisitiza umuhimu wa kueleza Ushia kwa usahihi mbele ya upotoshaji. Alieleza kuwa kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, dunia haikuufahamu Ushia kama ilivyostahili; taarifa nyingi zilizokuwepo zilitokana na maandiko ya Ahlus-Sunnah yaliyo na taarifa zisizokamilika au kwa makusudi kutoeleza Ushia kwa usahihi, na hivyo Ushia / Mashia walichukuliwa kama kundi dogo au la upande mmoja.
-
Pakistan Yatambuliwa Rasmi kama Mlinzi wa al-Haramain al-Sharifain
Rais wa Shirikisho la Vyuo vya Kiislamu vya Shia nchini Pakistan, Ayatullah Hafidh Sayyid Riaz Hussain Najafi, amelipongeza makubaliano ya ulinzi kati ya Saudi Arabia na Pakistan akiyataja kuwa hatua chanya na yenye kuleta matumaini.
-
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Ayatullah Akhtari kwa Sayyid Abdul Malik al-Houthi: Shambulio la Israel Nchini Yemen ni Jinai Mpya ya Kivita
"Ninatoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wa Yemen mashujaa na kwa uongozi wake jasiri – ukiwemo wewe ndugu yetu mpendwa, Sayyid Abdul Malik – kwa msiba huu mkubwa wa kifo cha Shahidi Ahmad Ghalib al-Rahwi na wenzake waliouawa kwa udhalimu na usaliti wa utawala haramu wa Kizayuni.”