31 Agosti 2025 - 18:15
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Ayatullah Akhtari kwa Sayyid Abdul Malik al-Houthi: Shambulio la Israel Nchini Yemen ni Jinai Mpya ya Kivita

"Ninatoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wa Yemen mashujaa na kwa uongozi wake jasiri – ukiwemo wewe ndugu yetu mpendwa, Sayyid Abdul Malik – kwa msiba huu mkubwa wa kifo cha Shahidi Ahmad Ghalib al-Rahwi na wenzake waliouawa kwa udhalimu na usaliti wa utawala haramu wa Kizayuni.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tehran: Ayatullah Muhammad Hassan Akhtari, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s), amemtumia ujumbe rasmi wa rambirambi Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen, kufuatia kuuawa shahidi kwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi ya Yemen, Ahmad Ghalib al-Rahwi, pamoja na mawaziri wengine waliouawa katika shambulio la anga la kinyama la utawala wa Kizayuni dhidi ya mji mkuu wa Sana’a.

Sehemu ya Ujumbe:

“Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

"Ninatoa ambirambi zangu za dhati kwa watu wa Yemen mashujaa na kwa uongozi wake jasiri – ukiwemo wewe ndugu yetu mpendwa, Sayyid Abdul Malik – kwa msiba huu mkubwa wa kifo cha Shahidi Ahmad Ghalib al-Rahwi na wenzake waliouawa kwa udhalimu na usaliti wa utawala haramu wa Kizayuni.”

Ayatullah Akhtari ameeleza kuwa shambulio hilo ni jinai ya wazi ya kivita na ya kinyama, inayoongeza ukurasa mwingine wa damu katika historia ya uhalifu wa utawala wa Kizayuni ,- kuanzia Gaza, Lebanon, Syria hadi Yemen na Iran - dhidi ya watu wasio na hatia.

Yamenaswa katika Ujumbe Wake:

  • Kusifu msimamo wa kishujaa wa Yemen katika kuunga mkono taifa la Palestina.
  • Kutoa heshima kwa muqawama wa Yemeni unaoendelea kuandika historia ya kujitolea kwa ajili ya Waislamu wa Palestina na harakati ya Kiislamu ya ukombozi.
  • Kulaani ukimya wa viongozi wa Kiarabu waliodhoofishwa na ushawishi wa Kizayuni.
  • “Tunayo yakini kuwa shambulio hili halitaivunja azma ya taifa la Yemen, bali litazidi kuimarisha msimamo wake wa ujasiri na uungaji mkono kwa muqawama wa Kiislamu.”

Katika hitimisho la ujumbe, Ayatullah Akhtari amenukuu Qur’an Tukufu akisema:

"Ikiwa mtamnusuru Mwenyezi Mungu, Atakusaidieni na kuimarisha miguu yenu." (Surat Muhammad, aya ya 7)


Imetolewa na: Ayatullah Muhammad Hassan Akhtari
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya AhlulBayt (a.s)
Mwenyekiti wa Kamati ya Uungaji Mkono kwa Mapinduzi ya Palestina – Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha