"Unaweza kumdhulumu mtu na ukalala usingizi mzito, lakini yule uliyemdhulumu halali kamwe. Anakumbuka dhulma yako kila siku na humlalamikia Mwenyezi Mungu dhidi yako. Na ikumbukwe kuwa macho ya Mwenyezi Mungu hayalali,” amesema Sheikh Ahmad Haji, akisisitiza hatari ya dua ya aliyedhulumiwa.
Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.