Utambulisho
-
Mkutano wa Kundi la Viongozi wa Kidini wa Kishia na Askofu Mkuu Mpya wa Washington
Kikundi cha viongozi wa kidini wa Kishia nchini Marekani pamoja na Askofu Mkuu wa Washington wamekutana katika kikao cha kirafiki ili kuimarisha ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo na kupanua njia za mazungumzo ya baina ya dini mbalimbali.
-
Jukumu la Marajii wa Kidini wa Kishia katika;
"Kulinda Umoja wa Kitaifa na Utambulisho wa Iran / Sehemu ya Saba: Kisa cha Kuokolewa kwa Lugha ya Taifa ya Iran na Ukombozi wa Azarbaijan"
Kulinda umoja wa ardhi na kuzingatia utambulisho wa kidini ni miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakipewa umuhimu mkubwa na viongozi wa kidini katika ardhi za Kiislamu. Kiasi kwamba kila aina ya uvamizi au shambulio dhidi ya ardhi za Kiislamu ilikabiliwa na mwitikio mkali kutoka kwao. Uvamiuzi wa Azarbaijan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na juhudi za kuutenga mkoa huo kutoka Iran ni miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha tena ushawishi wa uongozi wa kidini katika kulinda umoja wa ardhi ya nchi. Aidha, kulinda utambulisho wa kitaifa wa Kiairani pia lilikuwa ni mojawapo ya masuala yaliyopatiwa umuhimu maalum na viongozi (Marajii) wa kidini katika kipindi cha utawala wa Pahlavi.
-
Wakati Wanaume Wanaponyamaza, Dunia Hufa Kimyakimya
Wakati maana ya “uanaume” inapopotea, mwili nao hujibu. Kupungua kwa homoni ya testosterone, kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume (sperm), na kuzorota kwa uwezo wa kuzaa, si matokeo ya kibaolojia pekee — bali ni ishara ya kimya ya kupotea kwa dhamira ya uanaume. Mwanaume ambaye hajui kwa nini anapaswa kusimama, hatimaye hupoteza uwezo wa kusimama kabisa.
-
Nafasi ya Marājiʿ wa Kishia katika Kulinda Umoja wa Ardhi na Utambulisho wa Kitaifa- Sehemu ya 2 | Marāji ni, Walinzi wa Uhuru wa Nchi za Kiislamu
Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.
-
Infografia | Utambulisho wa Qā’im wa Aal Muhammad (s.a.w.w) katika Khutba ya Ghadir (9)
"Tambueni! Hakika mwisho wa Maimamu kutoka kwetu ni Qā’im al-Mahdi...Hakika yeye ndiye Hujja aliyebakia, na baada yake hakuna hujja mwingine".