Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Serikali ya Mali imetangaza kuwa raia wa Marekani wanaotembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi sasa watalazimika kulipia ada ya hadi dola 10,000 za Marekani (takribani shilingi milioni 24 za Kitanzania) kwa ajili ya viza za biashara na utalii.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni jibu la kisiasa kwa masharti mapya yaliyowekwa na utawala wa Rais Donald Trump, unaowataka raia wa Mali wanaotembelea Marekani kulipa ada kubwa za viza.
Kwa mujibu wa ubalozi wa Marekani nchini Mali, ada hiyo inalenga kuimarisha “dhamira ya Marekani ya kulinda mipaka yake na usalama wa taifa.”
Hata hivyo, wizara ya mambo ya nje ya Mali ilitoa taarifa siku ya Jumapili ikibainisha kuwa uamuzi huo wa Marekani ni wa upande mmoja, na kwa msingi huo, Serikali ya Mali imeamua “kuanzisha utaratibu wa viza wa kisawa” kwa raia wa Marekani wanaoingia nchini humo.
Your Comment