Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hezbollah imemtumia ujumbe Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ikimpa pole na kumpongeza kwa kuuawa shahidi kwa baba yake, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, huku ikitangaza utii wake na kuahidi kuendelea na njia ya Muqawama na jihadi chini ya uongozi wake.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mwenye kuwatukuza Waumini na kuwadhalilisha madhalimu, ambaye ameifanya maisha yetu kuwa jihadi na maandalizi, na mauti yetu kuwa kuuawa shahidi katika njia Yake kwa mikono ya viumbe Wake waovu zaidi. Rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, na kizazi chake kitukufu na chema. Na Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yao tukufu, nasi tukiwa katika kheri na afya njema.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume, na wenye mamlaka miongoni mwenu...” (An-Nisaa: 59)
Ama baada ya hayo...
Bwana wetu, Mheshimiwa Imam Kiongozi na Waliyy al-Faqih, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, Mwenyezi Mungu amlinde, amani, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako.

Sisi ni wana wenu na ndugu zenu wa Khamenei katika Hezbollah - Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon. Tunakutumia ujumbe huu huku nyoyo zetu zikiwa zimejaa matumaini na matarajio kwamba mko katika hali njema na afya kamili, mkilindwa na ngao imara ya Mwenyezi Mungu na ngome Yake madhubuti.
▪️Kwanza, tunakupongeza kwa kuuawa shahidi kwa baba yetu, Waliyy Shahidi, ambaye kwa kuuawa kwake shahidi alihitimisha miongo kadhaa ya jihadi na uongozi, akiwa ameunganisha elimu na matendo, akifungua milango ya utoaji akiwa faqihi mwenye maarifa, mwenye fikra za Qur’ani na kiongozi aliyeongozwa kwa usahihi, hadi alipouawa shahidi kama babu yake, shujaa wa mashambulizi, kwa mikono ya “Muljim” wa zama hizi / - (Kwa Mikono ya “Wamuljim wa zama hizi” kwa maana: Wale wanaofanana na Ibn Muljim katika zama hizi, na ibn Muljim Ndiye aliyemuua Imam Ali bin Abi Talib -as-).
Pia tunakupongeza kwa kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kujitolea kwa ndugu zenu na dada zenu, wana wenu wa kiume na wa kike, miongoni mwa wapiganaji wa kujitolea wa Umma huu katika uwanja wa Muqawama, hususan wana wa nchi yenu tukufu iliyo karibu na nyoyo zetu, Iran ya Kiislamu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awafunike mashahidi kwa rehema Zake, awajaalie majeruhi wapone haraka, na azijaalie familia zao subira na faraja.
⏺️ Sisi ambao kwa muda mrefu tumekuwa tukielekea katika mji mtakatifu wa Mashhad na kunywa kutoka katika chemchemi ya Imam mwenye huruma (a.s.) maji safi ya Wilaya, na huku tukiinua bendera ya Hussein (a.s.) kwa mkono wa jihadi na maandalizi, na kupambana na maadui zetu kutoka umbali wa sifuri, ambao maana yake ni “Labbaik na kamwe hatutakubali udhalilishaji”, kwa mkono mwingine tunawasalimu ndugu zetu wapendwa, wana wa Imam Ridha (a.s.), wahitimu wa shule ya Imam Khomeini (q.s.), na wenye shahada ya Imam Khamenei (q.s.), wanaoinua bendera yenu tukufu, miongoni mwa wanachama wa Walinzi wa Mapinduzi, Basij Tukufu, na kila mtu mwenye heshima na msimamo anayenusa harufu nzuri ya Wilaya katika Iran ya Kiislamu. Tunawaona ndani yao mapenzi na kujitolea kwa Imam Hussein (a.s.), uoni wa kina na kujitolea kwa Abbas, pamoja na yakini na uaminifu wa Salman.
▪️ Na leo hii, umebeba bendera ya Uislamu halisi wa Muhammadi, ambayo Waliyy Shahidi aliibeba baada ya Imam Khomeini Mkuu. Hii ndiyo bendera ambayo Imam Hussein (a.s) aliinua siku moja huko Karbala, alipokuwa peke yake mbele ya majeshi ya maadui na kuwapigia kelele kwa ulimi wa heshima na msimamo: “Wallahi, sitawapa mkono wangu kama mtu aliyedhalilika...”
⏺️ Ewe Kiongozi wetu, sisi kutoka ndani ya uwanja wa mapambano tunamopigana vita yetu ya Karbala dhidi ya Mafirauni wa dunia, tunakunyooshea mkono wa kiapo cha utii, kwa nguvu na azma yote. Sote tuna yakini kwamba kwa kufanya hivyo tunatoa kiapo cha utii kwa Imam Hujjat (a.j.), kwa kuwa wewe ni Naibu wake wa haki na hoja yake juu yetu katika zama za Ghaiba Kubwa.
▪️ Tunakuahidi kuendelea mbele katika njia ya “heshima”, tukiwa waandaaji na wenye subira. Kama tulivyokuwa pamoja na Waliyy Shahidi, tutakuwa pamoja nawe. Hatuogopi lawama za mwenye kulaumu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwenye shingo zetu kuna amana ya mashahidi, majeruhi, wafungwa na waliopotea pamoja na familia zao zenye subira. Na katika nyoyo zetu kuna njia ya Khamenei Shahidi, ambayo kaulimbiu yake ni nguvu na uwezo pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu.
⏺️ Chini ya uongozi wako, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tutasonga mbele katika uwanja wa mapambano tukiwa tumebeba bendera ya Uislamu kwa mwongozo wa Qur’ani na Ahlul-Bayt (a.s.), na jua letu likiwa ni Mahdi (a.j.), pamoja na viongozi wetu mashahidi waliotutangulia katika njia hii. Hatutaona upweke katika njia ya uongofu tukiwa pamoja na misafara ya mashahidi, majeruhi, akina mama, akina baba, wake na waume, pamoja na wana na mabinti wote wa Umma wa Muqawama na mbele ya jihadi.
Tutasonga mbele chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wetu, Mheshimiwa Sheikh Mujahid Naim Qassem, Mwenyezi Mungu amlinde. Matumaini yetu ni makubwa katika ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kurithi ardhi na kuidhihirisha dini Yake, chini ya uongozi wa Mansur kutoka katika kizazi cha Muhammad (a.s.). Na hadi ahadi hiyo itimie, kutoka kwetu hutaona chochote isipokuwa utiifu, azma ya ushindi na mapenzi ya kuuawa shahidi.
“Na ushindi hautoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye Hikima.”
Na mwisho wa dua yetu ni: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu.
Watoto wako na ndugu zako katika Hezbollah - Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon
Maoni yako