Wanafunzi Mabinti 144 wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo chini ya Jamiat Al-Mustafa - Tanzania, pamoja na wasimamizi wao, wamehuisha Majlisi ya kuomboleza Shahadat ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbala, ikiwa ni siku ya 30 ya maombolezo yanayo endelea katika Hawzah ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Dar es Salaam, Tanzania — Kwa mujibu wa taarifa, majlisi ya maombolezo ya Imam Hussein (a.s.) na Mashahidi wa Karbala imefanyika katika siku ya 30 ya mlolongo wa maombolezo kwa ajili ya Mashahidi wa Karbala, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza kumbukumbu ya tukio la A'shura na kujifunza mafunzo ya mapambano ya haki dhidi ya batili.
Katika majlisi hiyo, jumla ya wanafunzi 144 wa Hawza pamoja na wasimamizi wao walishiriki katika shughuli hiyo ya maombolezo, iliyoandaliwa na Hawzah ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni, Jijini Dar-es-salaam - Tanzania.
Majlisi hiyo ililenga kuhuisha kumbukumbu ya Imam Hussein (a.s.) na Mashahidi wa Karbala, pamoja na kuimarisha mafundisho ya kujitolea, kusimama kwa ajili ya haki na kupigania maadili ya Kiislamu.
Maoni yako