ushindi
-
Operesheni ya Kisaikolojia huko Karbala: Uchambuzi wa Kihabari wa Ujumbe wa Imam Hussein (a.s) kabla na baada ya Ashura
Mapinduzi ya Imam Hussein (a.s) hayakuwa vita vya kijeshi pekee; bali yalikuwa vita kamili vya kihabari na kisaikolojia vilivyolenga nyoyo na akili za watu. Kuanzia mahubiri ya Makka hadi ujumbe ulioandikwa kwa damu huko Karbala, Imam Hussein (a.s) aliwezaje kuhamasisha maoni ya umma dhidi ya utawala wa Yazid? Uchambuzi wa mkakati wa mawasiliano wa Imam (a.s) katika mojawapo ya nyakati nyeti zaidi katika historia ya Kishia, unaonesha mfano wa kipekee wa uanaharakati wa kihabari unaosimama juu ya ukweli.
-
Ushindi wa Jukwaa la Upinzani (Muqawama) ni Kudhihirika kwa Utabiri wa Qur’an
Kushindwa kwa Israel na Marekani katika mapambano ya hivi karibuni kunatokana na uongozi wa busara wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Mahakama Kuu Yaweza Kuongeza Ufanisi wa Mfumo wa Kiislamu Kupitia Utekelezaji wa Haki
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s), akiwa mbele ya wakurugenzi na wafanyakazi wa Mahakama ya Mkoa wa Gilan, amesema kuwa utekelezaji sahihi wa haki na usawa katika taasisi zote za serikali unaweza kuongeza ufanisi wa Jamhuri ya Kiislamu na kuthibitisha madai yake ya msingi kuhusu haki katika utawala.
-
Mazishi ya Mashahidi 300 Wasiojulikana Kufanyika Siku ya Kumbukumbu ya Shahada ya Bi.Fatima(sa); Dalili ya Umoja wa Kitaifa Baada ya Vita vya Siku 12
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC) wa Mkoa Mkuu wa Tehran, Sardar Hassanzadeh, amesema kuwa miili ya mashahidi 300 wasiojulikana—ikiwa ni pamoja na 200 kwa mikoa mbalimbali na 100 kwa jiji la Tehran—iko tayari kwa ajili ya mazishi ya kitaifa. Mazishi haya yatafanyika Jumatatu tarehe 3 Azar, sambamba na kumbukumbu ya shahada ya Bibi Fatima Zahra (a.s), ambapo msafara maalumu wa “Lale za Fatima” utaanza saa 2:00 asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran kuelekea kwenye kituo cha "Meraje’ Shohada".
-
Katika mahojiano na ABNA na mwanafalsafa wa Marekani: Kutoka ‘Medina’ hadi New York; Kushindwa kwa Ukuta wa Hofu Dhidi ya Uislamu Marekani
Profesa Charles Taliaferro, profesa mwandamizi wa falsafa katika Chuo cha Saint Olaf, akitaja wimbi la kampeni za propaganda za kupinga Uislamu nchini Marekani, alisema: “Licha ya kuwepo kwa baadhi ya vipengele vya kupinga Uislamu katika jamii ya Marekani, kuna ishara wazi za heshima, utu, na kukubaliana kati ya Waislamu na watu wengine. Ushindi wa Zahran Mamdani katika uchaguzi wa manispaa ya New York ni tukio muhimu katika kuimarisha harakati za kudhoofisha mazungumzo ya hofu dhidi ya Uislamu.”
-
“Ni Nani Mshindi Halisi?” – Wachambuzi wa Mashariki ya Kati Wajadili Makubaliano ya Kusitisha Vita Kati ya Hamas na Israel
Makubaliano Kati ya Hamas na Israel yameleta mabadiliko makubwa ya kimkakati, huku Hamas ikionekana kuibuka na ushindi wa kisiasa na kisaikolojia licha ya gharama kubwa za kibinadamu.
-
Mashambulizi ya Kipuuzi Zaidi Kufuatia Kuongezeka kwa Umaarufu na Ushindi wa Mamdani katika Uchaguzi wa Awali wa Umeya wa New York
Zahran Mamdani, Mbunge wa jimbo na mgombea wa chama cha Demokratik katika uchaguzi wa Umeya wa New York, kupitia kampeni za wananchi amefanikiwa kuwashinda wapinzani maarufu kama Andrew Cuomo katika kinyang’anyiro cha awali na kuwa mgombea wa kwanza Mwislamu kwa nafasi hiyo. Ushindi huo, hata hivyo, umekumbwa na mashambulizi ya chuki na matusi ya Uislamu kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, lakini yeye pamoja na wafuasi wake wametangaza kuwa hawatarudi nyuma mbele ya chuki na ubaguzi.
-
Katika mazungumzo na ABNA:
Ushuhuda wa Dada wa Shahidi Abbas Mousavi Kuhusu Kiongozi wa Muqawama:Syed alikuwa Mpenzi wa Mungu -Tulipata nguvu na matumaini kutoka kwa hotuba zake
Bi Hoda Mousavi, dada wa shahidi Sayed Abbas Mousavi, Katibu Mkuu wa zamani wa Hezbollah Lebanon, amesema: Sisi daima tulihisi katika maneno na mwongozo wake kwamba yeye kwanza kabisa alikuwa mpenzi wa Mungu. Mara tu tuliposikiliza hotuba zake, tulivutiwa kimagnet kwa hisia kwake; siri ya hilo ilikuwa katika ikhlasi na uaminifu wake kwa mpenzi wake wa kimungu.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mieleka ya Greco-Roman kwa ushindi wao wa ubingwa wa dunia
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michezo ya nchi yetu ambapo Timu ya Taifa ya mieleka ya “freestyle” na “Greco-Roman” zimefanikiwa kwa pamoja kutwaa ubingwa wa dunia katika mashindano moja.
-
Pakistan Yatambuliwa Rasmi kama Mlinzi wa al-Haramain al-Sharifain
Rais wa Shirikisho la Vyuo vya Kiislamu vya Shia nchini Pakistan, Ayatullah Hafidh Sayyid Riaz Hussain Najafi, amelipongeza makubaliano ya ulinzi kati ya Saudi Arabia na Pakistan akiyataja kuwa hatua chanya na yenye kuleta matumaini.
-
Sehemu ya Kwanza:
Miaka 120 ya Mapambano ya Familia ya Khamenei | Kizazi cha Upinzani na Mapambano | “Ninajivunia Kwamba Huyu Mtu Mashuhuri ni Babu Yangu"
Msimamo wa kupinga dhuluma na mapambano umekuwa miongoni mwa sifa kuu za familia ya Khamenei tangu karne zilizopita hadi sasa. Ingawa hakuna historia iliyoandikwa rasmi kuhusu mapambano ya familia hii, kuna ushahidi wa kihistoria na vielelezo vya wazi vinavyoonyesha kuwepo kwa historia ya miaka 120 ya mapambano yao.
-
-
Rais wa Iran: Mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran Yameleta Umoja wa Kitaifa Usio na Mfano
"Leo tunashuhudia kwa macho yetu kuwa kila Muirani - awe ni mfuasi wa Serikali au mpinzani wake - amekuwa sauti moja katika kutetea hadhi, uhuru, na mamlaka ya nchi yetu".
-
Waziri wa Ulinzi kwa Mwenzake wa Russia: Uamuzi wa Iran ni Kuadhibu Mchokozi kwa Nguvu Zote
"Kilicho hakika ni kwamba hatupigani na Israel pekee, bali tunapigana na Amerika na baadhi ya nchi pia (vibaraka) zinazoiunga mkono Israel."
-
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: Iran Imeshinda Vita
"Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali na watu wa Iran kwa ushindi huu".
-
Vyombo vya habari vya Kizayuni: Iran imeiongoza na kuisukuma Israel kuelekea kwenye kushindwa kimkakati
Vyombo vya habari vya Kizayuni vikichambua vimesema kuwa: Silaha za nyuklia ni hatari, lakini hisia ya ushindi katika mioyo ya maadui ni hatari zaidi.
-
Rais wa Israel: Tumelipa gharama kubwa katika vita na Iran - Hatujapata Ushindi wowote
"Tel Aviv imelipa gharama kubwa mno katika damu ya wakaazi (walowezi wa kizayuni) wa maeneo ya Israel (bali ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel) katika vita na Iran".
-
Wanafunzi wa Madrasatul Hizbullah Al-‘Ilmiyyah Wafanya Mtihani wa Mwisho wa Mwezi - Kazole, Vikindu
Madrasatul Hizbullah Al-‘Ilmiyyah inatoa wito kwa jamii kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo ili iweze kuendelea kutoa elimu bora na kukuza kizazi chenye maarifa, hikma na hofu ya Mwenyezi Mungu.
-
Kwa mujibu wa Qur'an Tukufu: Kundi la Mwenyezi Mungu, linalomtii Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waliokuwa Waumini wa kweli, Hao ndio washindi wa kweli
"Hezbollah" humaanisha: Kundi lililojifunga na miongozo ya Mwenyezi Mungu, linalosimama na kutetea haki, hata likiwa ni dogo au linakabiliwa na maadui wakubwa. Aya hii imekuwa nembo ya Harakati za Muqawama (Upinzani wa Kiislamu) kama vile Hezbollah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, na wengineo wanaopambana dhidi ya dhulma ya mabeberu ya Kimataifa.
-
Dalili ya wazi na kubwa Kuhusu Kupigana kwa Malaika Pembeni ya Ali (as)
kwa Hakika Amirul-Mu'minin Ali (a.s) hakuwa anarudi kutoka vitani mpaka apate ushindi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Na ni fadhila iliyo kubwa kiasi gani kuwa Malaika Jibril (as) anapigana upande wa kulia wake, na Mikail (as) upande wa kushoto wake.