Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Ulinzi wa Iran Amir Nasirzadeh, Waziri wa Ulinzi wa Russia alitoa salamu za rambirambi kwa kuuawa shahidi kundi la makamanda wa ngazi za juu wa kijeshi na raia wa Iran na kusema: "Shambulio katika ardhi ya Iran katika kadhia ya nyuklia si chochote ila ni kisingizio, na wanataka kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueneza machafuko katika eneo zima." Urusi inafuatilia maendeleo yote na itaiunga mkono Iran.
Amir Nasirzadeh, huku akiishukuru Urusi kwa uungaji mkono wake kwa Iran, alisema: "Kilicho hakika ni kwamba hatupigani na Israel pekee, bali tunapigana na Amerika na baadhi ya nchi pia (vibaraka) zinazoiunga mkono Israel." Uamuzi wetu ni kumwadhibu mchokozi kwa nguvu zetu zote, na hatutakubali amani iliyowekwa.
Chanzo cha matatizo yote na ukosefu wa utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati, ni Marekani na Israel. Tunaweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani na utulivu katika eneo hili la kikanda na dunia nzima kwa ujumla.
Your Comment