Mashariki ya Kati
-
Mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa Auawa Shahidi katika Shambulio la Kigaidi Kusini-Mashariki mwa Iran
Mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ali Ibn Abi Talib, Molavi Mohammad Anwar Rigi, ameuawa Shahidi baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana katika mji wa Mirjaveh, kusini-mashariki mwa Iran. Mamlaka za eneo hilo zimesema uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa shambulio hilo, huku wananchi wakitakiwa kudumisha utulivu na kutoruhusu tukio hilo kuchochea migawanyiko ya kidini.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi Awasili Oman kwa Mazungumzo kuhusu Mlango Bahari wa Hormuz na Hali ya Kanda ya Mashariki ya Kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amewasili mjini Muscat, Oman, kwa ziara ya kidiplomasia inayolenga kujadili usimamizi wa Mlango wa Hormuz, maendeleo ya kikanda na kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Oman.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia Wafanya Mazungumzo kwa Simu Kujadili Hali ya Kanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araqchi, na mwenzake wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan, wamejadili kwa njia ya simu maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda kufuatia hatua za uhasama zilizochukuliwa na Marekani.
-
Jeshi la Iran: Mtu au Eneo Lolote Litakalosaidia Vikosi vya Marekani Litachukuliwa kuwa Lengo Halali
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa onyo kwamba mtu, kituo au eneo lolote litakalotoa msaada kwa vikosi vya Marekani katika mashambulizi dhidi ya Iran litachukuliwa kuwa lengo halali la vikosi vya Iran.
-
Mshauri wa Kamanda wa IRGC: Mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Yatakuwa Chachu ya Mabadiliko Makubwa Kanda ya Mashariki ya Kati
Mshauri wa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, yatakuwa hatua muhimu itakayochochea maendeleo na mabadiliko ya kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq: Baghdad Ina Uhusiano Bora Sana na Tehran na Iko Tayari Kusaidia Kumaliza Vita
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein, amesema kuwa Iraq ina uhusiano mzuri na Iran na Marekani, huku akisisitiza kuwa Baghdad iko tayari kushirikiana na pande zote mbili ili kumaliza vita na kuimarisha amani katika eneo hilo.
-
Rais Pezeshkian: Sera za Kivamizi za Utawala wa Kizayuni Ndizo Chanzo cha Ukosefu wa Usalama katika Eneo
Rais Masoud Pezeshkian amesema sera za uchokozi za utawala wa Kizayuni ndizo chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika eneo, huku Iran na Serbia zikisisitiza umuhimu wa kuimarisha amani, utulivu na ushirikiano wa pande mbili.
-
Rais wa Falme za Kiarabu Apongeza Makubaliano ya Marekani na Iran na Kusisitiza Amani ya Kudumu Mashariki ya Kati
UAE yaunga mkono makubaliano ya Marekani na Iran, ikisisitiza amani ya Mashariki ya Kati ijengwe juu ya heshima ya mamlaka ya mataifa na sheria za kimataifa.
-
Mchambuzi wa Zamani wa CIA: Marekani na Israel Zinajaribu Kuhujumu Mazungumzo na Iran
Mchambuzi wa zamani wa CIA Larry Johnson amesema mashambulizi dhidi ya Iran wakati mazungumzo yakiendelea yanaashiria juhudi za kuhujumu mchakato wa kidiplomasia, akionya kuwa huenda eneo hilo likashuhudia duru mpya ya mvutano katika siku zijazo.
-
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi: Marekani Itakubali Masharti ya Iran au Ikabiliwe na Matokeo Makubwa
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran ameonya kuwa Marekani italazimika kukubali masharti ya Tehran au kukabiliwa na matokeo makubwa, akiihusumu Washington kwa kuhujumu diplomasia na kutoheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
WSJ Yadai UAE Ilifanya Mashambulizi ya Anga Dhidi ya Iran Wakati wa Vita
Ripoti ya Wall Street Journal imedai kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu ulifanya makumi ya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran kuanzia siku za mwanzo za vita na kuendelea hadi baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano mwezi Aprili, madai yaliyoibua mjadala kuhusu nafasi ya mataifa ya Ghuba katika mzozo huo.
-
Onyo la Kataib Hezbollah Iraq kwa Marekani kuhusu Kuanzisha Vita katika Eneo
Kataib Hezbollah imeonya kuwa iwapo Marekani itaanzisha vita katika eneo hilo, itakabiliwa na hasara kubwa na vita vya muda mrefu, huku pia ikiutahadharisha utawala wa Kurdistan kuepuka kushirikiana na majeshi ya kigeni.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi Aongoza Ujumbe wa Mazungumzo na Marekani Muscat
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameongozana na ujumbe wake wa kidiplomasia kuelekea mjini Muscat, Oman, kwa ajili ya mazungumzo na Marekani. Mazungumzo hayo yanatazamwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kujadili masuala ya nyuklia, vikwazo vya kiuchumi na usalama wa kikanda, kwa lengo la kufungua ukurasa mpya wa maelewano ya kisiasa.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Akutana na Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kishia Lebanon Beirut
Wakati wa ziara yake rasmi mjini Beirut, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, alikutana na Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon. Mazungumzo yao yalijikita katika maendeleo ya kikanda, umuhimu wa umoja wa Kiislamu, na kuimarisha ushirikiano wa kidini na kisiasa kwa ajili ya uthabiti na mshikamano wa Lebanon.
-
Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu
"Uwezo wetu wa kijeshi unalenga kuzuia uchokozi na kulinda mamlaka, ardhi na maslahi ya taifa la Iran"
-
Turki Al-Faisal: Tishio Kuu la Mashariki ya Kati Sio Iran, Bali ni Israel
Shambulizi Dhidi ya Ujumbe wa Hamas Qatar ni Onyo kwa Nchi za Ghuba | Katika kauli yake nzito, Turki Al-Faisal pia amebainisha kuwa shambulizi la Israel dhidi ya ujumbe wa Hamas nchini Qatar lilikuwa ujumbe wa vitisho kwa nchi za Ghuba, akisema hatua hiyo ilikuwa onyo la wazi kuwa mataifa ya Ghuba yako katika hatari na yanapaswa kuchukua tahadhari za pamoja za kiulinzi.
-
Kifo cha mtu aliyebuni / aliyeratibu vita - Dick Cheney na urithi mbaya na mchungu wa Iraq
Kwa kifo cha Dick Cheney, makamu wa rais wa zamani wa Marekani, tena uso mmoja unakumbukwa ambaye jina lake limeunganishwa na Vita vya Iraq, mateso, na mabadiliko ya sura ya siasa za Marekani katika Mashariki ya Kati.
-
Trump Aondoka Mashariki ya Kati Bila Kujibu Maswali Muhimu
Rais wa Marekani ameondoka katika eneo hilo bila kutoa majibu kwa maswali yaliyoibuliwa kabla ya kuwasili kwake. Hali hii imeacha ukosefu wa uwazi kuhusu nia na mikakati ya Marekani katika eneo, huku wachambuzi wakibainisha kuwa maswali muhimu kuhusu sera za kisiasa na usalama hayajapatiwa majibu.