26 Juni 2025 - 21:19
Imam wa Msikiti wa Imam Sadiq (as), Mauritania: "Israeli ni uvimbe wa saratani ambao lazima uondolewe kabisa | Umoja wa Kiislamu uko juu ya Madhehebu"

Kauli hii ya Imam huyu inasisitiza umuhimu wa mshikamano wa Waislamu kote duniani, kwani umoja wa kweli unapaswa kuvuka mipaka ya tofauti za madhehebu na kuwa na lengo moja la kutetea haki na kuondoa dhuluma na udhalimu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Imam wa Msikiti wa Imam Sadiq (a.s) kutoka Mauritania amesema: "Israeli ni uvimbe wa saratani ambao lazima uondolewe kabisa; umoja wa Kiislamu ni jambo linalozidi mipaka ya madhehebu."

Kauli hii inaonyesha msimamo thabiti wa Imam huyu kuhusu hali ya utawala wa Kizayuni (Israel) na wito wa Umoja wa Kiislamu, bila kuendekeza fikra potovu za umadhehebu au itikadi tofauti zenye lengo la kudhaifisha Umoja wa Waislamu Duniani katika kumkabili adui wa Umma wa Kiislamu. 

Imam huyo, anasisitiza kuwa changamoto kubwa inayoikabili dunia ya Kiislamu ni kudumisha "Umoja wa Kiislamu" ili kumshinda adui wa pamoja, ambaye ni Israel - inayolinganishwa sawa na ugonjwa hatari wa saratani katika eneo la Mashariki ya Kati na Dunia kwa ujumla 

Kwa upande mwingine, wito huu Imam huyu unasisitiza umuhimu wa mshikamano wa Waislamu kote duniani, kwani umoja wa kweli unapaswa kuvuka mipaka ya tofauti za madhehebu na kuwa na lengo moja la kutetea haki na kuondoa dhuluma na udhalimu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha