3 Septemba 2025 - 11:39
Atlantic: Iran Yajenga Njia Mpya na Kuwapita Maadui Zake

Tabia ya ustahimilivu ya Iran na mhimili wa muqawama (mapambano ya upinzani) katika miongo iliyopita imeonyesha kuwa, licha ya mashinikizo na mashambulizi kutoka Marekani na utawala wa Kizayuni, Iran daima imeweza kujirekebisha kimkakati na kupata njia mpya za kukabiliana na changamoto.

Kwa mujibu wa shirika la habari la kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA- jarida la Marekani The Atlantic limeandika makala kuhusu mkakati wa kikanda wa Iran. Ingawa makala hiyo imejaribu kudhoofisha nguvu za Iran kwa kuonyesha hadithi ya "kuporomoka kwa ushawishi", uchambuzi makini unaonesha mambo kadhaa muhimu: uimara wa Iran, ushawishi wake wa muda mrefu katika eneo, na uendelevu wa utambulisho wa muqawama wa Jamhuri ya Kiislamu.

Jarida la Atlantic linarejelea mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran na washirika wake wa muqawama, lakini linamnukuu Michael Doran, mchambuzi kutoka Taasisi ya Hudson, akisema:

"Wamepata pigo, lakini hakuna dalili kwamba wataanguka."

Jarida hilo linakiri kuwa Iran imeweza kujinasua mara kwa mara kutoka kwenye hali ngumu kwa kupitia mapitio ya kimkakati na kuunda njia mpya za kuwapita Marekani na Israel — na kuna matarajio kuwa itafanya hivyo tena.

Katika makala hiyo, Atlantic pia imenukuu kauli ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, kuhusu uhalifu wa hivi karibuni wa Marekani na Israel, akisema:

"Mhimili wa muqawama si kama kifaa cha kielektroniki kinachoweza kuvunjwa au kuharibiwa. Hauwezi kudhoofishwa kwa mashinikizo — bali unazidi kuwa imara."

Mwanadiplomasia mmoja Mmarekani alisema kwenye mahojiano na Atlantic:

"Mkakati wa Iran bado unaendelea kufanya kazi. Nina hofu kwamba kabla hatujamaliza kazi yetu, tutapoteza kabisa ushawishi wetu katika eneo hili."

Jarida hilo linaendelea kufichua kuwa licha ya mapigo dhidi ya mhimili wa Muqawama, haujashindwa - bali katika kipindi cha miaka 20 iliyopita umekuwa ukiongoza mabadiliko ya kijiografia ya kisiasa na kuwa changamoto kwa mataifa tajiri ya Magharibi.

Katika kueleza ustahimilivu wa Muqawama, Atlantic limetaja uvamizi wa Marekani dhidi ya Iraq na mapambano ya Sayyid Muqtada al-Sadr, likimnukuu Ricardo Sanchez, kamanda wa zamani wa majeshi ya ardhini wa Marekani nchini Iraq, aliyesema:

"Lengo langu lilikuwa kumuua Muqtada Sadr, lakini huwezi kupuuza kwamba Sadr alikuwa akihutubia hadhara kubwa, huku mimi nikiwa najificha nikitoa matamko katika maficho."

Aidha, jarida hilo limetambua kuwa Harakati ya Hamas, licha ya miaka miwili ya mashambulizi na mzingiro wa Gaza, bado imesalia imara — na huo uwepo wake pekee ni "aina ya ushindi".

Kuhusu Iraq, makala hiyo inaonesha kuwa baada ya kuuawa kwa Shahidi Qassem Soleimani, makundi ya muqawama nchini humo yameendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa na uchumi wa nchi, huku mengi yakionesha uaminifu wao kwa Iran.

Ingawa makala inakiri kuwa mhimili wa muqawama unakabiliwa na hali ngumu, pia inakubali kwamba Iran ina uwezo wa kubuni mikakati mipya ya kukabiliana na maadui wake.

Mwishoni, Atlantic inakiri kwamba hata wakosoaji wa ndani wa Serikali ya Iran, katika nyakati za mapambano dhidi ya Marekani na Israel, huonesha mshikamano wa kitaifa na kusimama upande wa serikali yao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha