Tabia ya ustahimilivu ya Iran na mhimili wa muqawama (mapambano ya upinzani) katika miongo iliyopita imeonyesha kuwa, licha ya mashinikizo na mashambulizi kutoka Marekani na utawala wa Kizayuni, Iran daima imeweza kujirekebisha kimkakati na kupata njia mpya za kukabiliana na changamoto.
Wamagharibi hatwaki kuona Iran ikiwa ni nchi huru, na hii ni kutokana na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwatetea wananchi wa Palestina na kukataa udhalimu wa uvamizi wa Kizayuni kwa ardhi za Taifa la Palestina.