Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Kiongozi Mkuu wa Ansarullah - Yemen, Sayyid Abdul Malik Al-Huthi ameeleza kwamba nchi za Magharibi zinailenga Iran kwa sababu itikadi ya Iran ni kusimama imara katika kuihami Palestina, na haiajaacha kamwe kuwahami Wapalestina.
Marekani na Israel, wanamiliki silaha za Nyuklia, na kwa hakika wao ndio tishio la Jamii ya Wanadamu. Na ikiwa silaha za Nyuklia ni tishio la jamii ya wanadamu, basi kwa hakika wa kwanza ambaye anatakiwa kuzuiwa kumiliki silaha za nyuklia ni adui Israel.
Akifafanua sababu ya wamagharibi kufanya uadui dhidi ya Iran amesema:
Wamagharibi hatwaki kuona Iran ikiwa ni nchi huru, na hii ni kutokana na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwatetea wananchi wa Palestina na kukataa udhalimu wa uvamizi wa Kizayuni kwa ardhi za Taifa la Palestina.
Your Comment