Utawala wa Kizayuni ulilenga nyumba ya makazi na baadhi ya watu wa familia ya Hassan Badir pia walikuwa ndani ya nyumba hiyo wakati wa jinai hiyo ya Wazayuni.
Ayatollah Javadi Amoli, akiwaalika watu kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alisema:
Ni wajibu wetu sote kushiriki katika Maandamano haya, kwanza, Na kila mmoja wetu kwa mujibu wa elimu tuliyo nayo, awe na nia ya Tawalli na Tabarri ya Kimungu, pili, na kujaribu kufayanya kuwa maandamano mapana zaidi, tatu, yaani tuyafanye maandamano haya kwa nia ya kuwa karibu na kuwaheshimu na kuwathamini Mashahidi wa njia hii, ili hatua hizi zote zithibitishwe na Dhati Takatifu ya Mwenyezi Mungu.