Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Hassan Badir (anayejulikana kwa jina la Haj Rabi), mmoja wa maafisa wa dawati la Palestina la Hezbollah nchini Lebanon, aliuawa Shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni kwenye viunga vya Mji wa Beirut, lililofanyika jana usiku kwa kulishambulia jengo la makazi kwa mashambulizi ya anga bila ya tahadhari ya awali.
Katika jinai hiyo, utawala wa Kizayuni ulilenga nyumba ya makazi na baadhi ya watu wa familia ya Hassan Badir pia walikuwa ndani ya nyumba hiyo wakati wa jinai hiyo ya Wazayuni. Mtoto wa Hassan Badir pia aliuawa Kishahidi katika shambulio hilo sambamba na baba yake Hassan Badir.
Your Comment