2 Aprili 2025 - 23:17
Shambulio baya la jeshi la Kizayuni kwenye Kliniki (Zahanati) ya Umoja wa Mataifa Kaskazini mwa Gaza

Shambulio la Wazayuni katika Zahanati moja katika Ukanda wa Gaza limepelekea kuuawa Shahidi watu kadhaa wakiwemo watoto.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Vyanzo vya habari vimeripoti kuhusu shambulio la jinai la utawala wa Kizayuni katika Zahanati ya "UNRWA" Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuua na kujeruhi makumi ya watu wakiwemo watoto kadhaa.

Kwa mujibu wa ripoti za vyanzo hivi, jeshi la Kizayuni limeishambulia Zahanati hii, ambayo ni ya Shirika la UNRWA, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza katika kambi ya Jabalia.

Watu 19 wameuawa Shahidi, 9 kati yao wakiwa ni watoto, kutokana na shambulio hilo la anga la utawala haram na ghasibu wa Kizayuni kwenye kituo hicho cha matibabu cha UNRWA huko Jabalia, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo wakimbizi wa Kipalestina walikuwa wakijihifadhi ndani yake.

Shambulio hili limetekelezwa baada ya Yasrael Katz, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni leo asubuhi kutangaza kupanuka kwa mashambulio mbalimbali katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, kuanzia Oktoba 7, 2023 hadi Juni 30, 2024, mashambulizi 136 katika Hospitali 27 na vituo vingine 12 vya Matibabu yalirekodiwa huko Gaza. Mashambulizi haya yamesababisha vifo vya kishahidi vya madaktari wengi, wauguzi pamoja na wafanyakazi.

Tangu Oktoba 2023, jeshi la Israel limeua zaidi ya Wapalestina 50,300 katika Ukanda wa Gaza na kuwajeruhi wengine zaidi ya 114,000. Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza kuwa, idadi ya Mashahidi ni kubwa zaidi kuliko takwimu zilizotangazwa, kwa sababu bado kuna mashahidi wengi wa Kipalestina chini ya vifusi na mitaani, maeneo ambayo haiwezekani kufikiwa katika hali ya vita.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha