20 Oktoba 2025 - 10:07
Serikali ya Ndani ya Palestina kuanza kufanya kazi kikamilifu Gaza ndani ya mwaka mmoja

Takribani robo ya majeruhi wa mashambulizi ya Israel wamepata ulemavu wa kudumu, na upatikanaji wa huduma na rasilimali katika eneo hilo bado ni mdogo sana.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -, ABNA- Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammad Mustafa, ametangaza kuwa Serikali ya Ndani ya Palestina (PA) itarejea kufanya kazi kikamilifu katika Ukanda wa Gaza ndani ya miezi 12 ijayo, huku mpango wa miaka mitano wa ujenzi upya na utoaji wa huduma mbalimbali ukiwa tayari umeandaliwa.

Tangu mwaka 2007, Serikali ya Ndani ya Palestina haijakuwa na usimamizi wa moja kwa moja katika Ukanda wa Gaza na imekuwa ikitoa huduma chache pekee.

Mustafa anatarajia kwamba ndani ya mwaka mmoja, serikali hiyo itakuwa imeanza shughuli kamili katika eneo hilo.

Mpango wa ujenzi upya unajumuisha sekta 18 ikiwemo makazi, elimu na usimamizi, na unahitaji takriban dola bilioni 65 za Marekani.

Wapalestina wamesisitiza mamlaka yao kamili juu ya Ukanda wa Gaza na wamesema ushiriki wa nchi za Kiarabu na jumuiya za kimataifa katika ujenzi utakuwa wa kiwango cha usaidizi pekee.

Hali ya afya katika Gaza ni ya dharura - hospitali 13 pekee ndizo zinazoendelea kutoa huduma kwa kiwango cha chini, huku magonjwa yakisambaa bila udhibiti.

Takribani robo ya majeruhi wa mashambulizi ya Israel wamepata ulemavu wa kudumu, na upatikanaji wa huduma na rasilimali katika eneo hilo bado ni mdogo sana.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha