Katika ripoti ya hivi punde kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza, Mwanaharakati wa Kipalestina amesema: "Kwa ujumla, zimepita takriban siku 45 tangu hata kilo 1 ya unga au chupa 1 ya maji iingie Gaza, na mzingiro huo uko katika hali mbaya zaidi."
Wakati huo huo hujuma zikiendelea na ugavi wa misaada kwa Gaza ukikatizwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto lilionya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hili na kutangaza kwamba maisha ya watoto wapatao milioni moja katika ukanda huu yako chini ya hatari na tishio kubwa.