9 Aprili 2025 - 11:40
Ripoti juu ya hali ya hivi punde huko Gaza / Kwa mara ya kwanza katika historia, watu milioni 2 wamezingirwa katika ukanda mmoja (Ukanda wa Gaza)

Katika ripoti ya hivi punde kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza, Mwanaharakati wa Kipalestina amesema: "Kwa ujumla, zimepita takriban siku 45 tangu hata kilo 1 ya unga au chupa 1 ya maji iingie Gaza, na mzingiro huo uko katika hali mbaya zaidi."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA-, Kila siku tunasikia habari za kuhuzunisha na picha za watu wa Gaza na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu katika maeneo tofauti ya mji huo. Kulingana na wakaazi wa Gaza, watu wa Mkoa huu wanaishi katika hali ngumu zaidi, na kwa mara ya kwanza, watu milioni 2 katika eneo la kilomita za mraba 200 wamezingirwa, na hata chupa ya maji haijaingia Gaza kwa takriban siku 45. Jinai zote hizo zinafanyika chini ya kivuli cha kimya cha kimataifa, na viongozi wa nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu, mbali na matamshi na mapendekezo yao hawachukui hatua yoyote ya kivitendo kusimamisha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza.

Ripoti juu ya hali ya hivi punde huko Gaza / Kwa mara ya kwanza katika historia, watu milioni 2 wamezingirwa katika ukanda mmoja (Ukanda wa Gaza)

"Moneim Muhammad," Mwanafunzi wa Kipalestina anayeishi Iran, alielezea hali ya hivi punde katika Ukanda wa Gaza kwenye chaneli yake ya kibinafsi ya anga ya mtandao, ambayo iliundwa ili kuwafahamisha hadhira yake kuhusu hali inayojiri huko Gaza:

Ukanda wa Gaza uko katika hali mbaya na kwa sasa umegawanywa katika maeneo matatu yenye hali tofauti.

Eneo la kwanza: Rafah, Mji wenye umri wa miaka 3,300 ambao unaunda asilimia 16 ya eneo la Gaza, ulikuwa nyumbani kwa Wapalestina 40,000 kabla ya vita. Katika mapigano hayo, jiji hilo likawa kimbilio la watu milioni 1 waliokimbia makazi yao, lakini sasa halijaachwa kabisa na kuharibiwa kwa mabomu na mashambulizi ya kijeshi.

Ripoti juu ya hali ya hivi punde huko Gaza / Kwa mara ya kwanza katika historia, watu milioni 2 wamezingirwa katika ukanda mmoja (Ukanda wa Gaza)

Wakaazi wa Rafah ama wameuawa Shahidi au wamekimbia makazi yao, na mji huu ulikuwa eneo la kwanza kukaliwa kwa mabavu katika Ukanda wa Gaza. Hapo awali Rafah ilikaliwa kwa mabavu kuanzia 1967 hadi 2005, hadi ilipokombolewa mwaka 2005 na watu wa Muqawamah (Upinzani) wa Gaza.

Eneo la pili: Ni Khan Younis na Deir al-Balah. Na eneo la tatu ni: Ukanda wa Kaskazini wa Gaza (Mji wa Gaza na Jabalia). Mikoa yote hiyo imeharibiwa vibaya mno kupitia utawala haram wa kizayuni.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha