utawala wa Kizayuni
-
Msemaji wa Serikali ya Iran: Wale waliotekeleza uhalifu huko Ghaza wanapaswa kufikishwa mbele ya Mahakama
Msemaji wa serikali, huku akionyesha unga mkono kwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ghaza, alisisitiza kuwa: kusitishwa kwa uhalifu wa utawala wa Israel huko Ghaza si mwisho wa safari, na wale waliotekeleza na waliyoamuru uhalifu huu wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama za kimataifa.
-
Sayyid Abdul-Malik al-Houthi: Uhalifu wa utawala wa Kizayuni unafanywa kwa msaada wa Marekani na kimya pamoja na kutochukua hatua kwa Waarabu
Mtazamo wa wazi wa Marekani inapozungumzia mabadiliko ya Mashariki ya Kati ni kubadilisha hali ya eneo hilo kwa manufaa ya adui wa Kizayuni kwa gharama ya uhuru, kujitegemea, heshima, dini na haki za mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.
-
Janga la Kibinadamu Gaza; Watoto Yatima Katika Hali ya Ndoto Mbaya
Janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza limeharibu maisha ya maelfu ya watoto. Watoto hawa wamekuwa wakikabiliana na hali ya kukimbia, njaa, kifo cha wapendwa, na vurugu za kutisha kwa takriban miaka miwili. Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 65,000 wamefariki Gaza, huku maelfu ya watoto wakipoteza wazazi wao. Hali hii ya ukosefu wa usalama na mahitaji ya msingi inatengeneza athari kubwa za kimahusiano na kisaikolojia kwa vizazi vijavyo, na kufanya msaada wa haraka wa kimataifa kuwa jambo la dharura. Watoto hawa yatima sasa wanahitaji hifadhi, chakula, huduma za afya na msaada wa kisaikolojia ili kuweza kuendelea na maisha yao.
-
Imamu Mkuu wa Baghdad amesisitiza umuhimu wa kushiriki kwa ufahamu katika uchaguzi wa Bunge la Wawakilishi wa Iraq | Nguvu ya Muqawama wa Hizbollah
Imamu Mkuu wa Baghdad alisema kuwa taifa la Iraq leo limekabiliwa na chaguo mbili: ama kukubali serikali dhaifu isiyoweza, ama kwa kushiriki kwa nguvu katika uchaguzi kuharibu mpango wa Marekani.
-
Mkutano wa Viongozi wa Iran na Iraq:
Pezeshkian: Waislamu wafanye jitihada kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni Al-Sudani: Juhudi za nchi za Kiislamu zisibaki kwenye matamko tu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri Mkuu wa Iraq wametoa msisitizo juu ya ulazima wa kuchukua msimamo mmoja wa pamoja kati ya nchi za Kiislamu, ili kuwe na hatua madhubuti na za vitendo za kusitisha na kuzuia marudio ya jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Netanyahu: "Tutaendelea Kuwalenga Viongozi wa Hamas"
Kiongozi wa serikali ya Kizayuni (Israel) katika mkutano wa waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, alitetea shambulio la uvamizi la taifa hilo dhidi ya Qatar lililolenga kuuwa viongozi wa Hamas, na hakukatisha nafasi ya kuonyesha kuwa shambulio kama hilo linaweza kurudiwa dhidi ya nchi nyingine za eneo.
-
Onyo kutoka kwa Kiongozi wa Ansarullah:
Kiongozi wa Ansarullah wa Yemen, akifichua ukubwa wa mauaji ya kimbari na uharibifu wa miundombinu huko Gaza, ametaja pia mipango ya upanuzi ya utawala wa Kizayuni katika eneo la kikanda, ikiwemo Lebanon, Syria na uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya Qatar. Ameitaja Marekani kuwa mshirika katika uhalifu huu na kusisitiza kuendelea kwa mapambano na mshikamano wa Kiislamu katika kukabiliana na uchokozi huu.
-
Pezeshkian: Madai ya Trump kuhusu kukomesha mpango wa Nyuklia wa Iran ni Udanganyifu
Katika mahojiano na gazeti la Al-Jazeera, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza utayarifu wake wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni, aliyataja mazungumzo ya kuhitimisha mpango wa nyuklia wa Iran kuwa ni ndoto na njozi. Aidha, alisema: Hatutaki Vita, lakini Tuko Tayari Kujilinda kwa Nguvu Zetu Zote.
-
Mafanikio mawili ya Yemen ndani ya siku moja; Mashambulizi ya Kimaonyesho dhidi ya Hodeidah yazimwa na kushindwa/Meli "Magic Seas" Yazamishwa Baharini
Yemen, imefanikiwa kuitwanga meli iliyokuwa ikielekea maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa Kizayuni, na kuizamisha baharini.
-
Wayahudi Wanaopinga Uzayuni Wametoa Pongezi kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Israel Dhidi ya Iran
Mayahudi wanao uchukia Uzayuni huko New York, walihudhuria katika Ofisi ya Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York na kutoa heshima zao kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni.
-
Ripoti juu ya hali ya hivi punde huko Gaza / Kwa mara ya kwanza katika historia, watu milioni 2 wamezingirwa katika ukanda mmoja (Ukanda wa Gaza)
Katika ripoti ya hivi punde kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza, Mwanaharakati wa Kipalestina amesema: "Kwa ujumla, zimepita takriban siku 45 tangu hata kilo 1 ya unga au chupa 1 ya maji iingie Gaza, na mzingiro huo uko katika hali mbaya zaidi."