23 Julai 2025 - 16:03
Pezeshkian: Madai ya Trump kuhusu kukomesha mpango wa Nyuklia wa Iran ni Udanganyifu

Katika mahojiano na gazeti la Al-Jazeera, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza utayarifu wake wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni, aliyataja mazungumzo ya kuhitimisha mpango wa nyuklia wa Iran kuwa ni ndoto na njozi. Aidha, alisema: Hatutaki Vita, lakini Tuko Tayari Kujilinda kwa Nguvu Zetu Zote.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Dk. Masoud Pezeshkian, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika mahojiano yake ya kwanza ya televisheni baada ya vita ya siku 12 dhidi ya Iran (katika mwezi Juni uliopita), amesema Iran iko tayari kukabiliana na harakati yoyote ya kijeshi kutoka kwa utawala haram wa Kizayuni, na kwamba madai ya Israel ya kuharibu mpango wa nyuklia wa Iran ni ndoto na njozi ya mchana. Alisisitiza akisema: "Hatutaki Vita, lakini Tuko Tayari Kujilinda kwa Nguvu Zetu Zote".

Matamshi Muhimu ya Rais Pezeshkian kwa Al Jazeera ni haya yafuatayo:

1- Kuhusu vita ya siku 12:

“Jeshi la Iran liko tayari kulenga maeneo ya kina kabisa ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Tuliitwanga na kuishambulia Israel kwa nguvu, lakini Tel Aviv inaficha kiwango cha hasara waliyoipata.”

2- Kuhusu ushindi wa Iran:

“Israel ilitaka kueneza vurugu na kuporomosha mfumo wa Kiislamu kupitia mashambulizi ya kijasusi na kisiasa, lakini imeshindwa.”

3- Kuhusu dhamira ya Iran:

“Hatutaki vita, lakini pia hatuamini kuwa kuna usitishaji wa vita wa milele. Tupo tayari kujilinda kwa uwezo wetu wote. Hatutasalimu amri.”

4- Kuhusu Mpango wa Nyuklia na Trump:

Pezeshkian amejibu madai ya Donald Trump kwamba “mashambulizi ya Marekani yameangamiza mpango wa nyuklia wa Iran”, kwa kusema:

“Hili ni wazo la kidhahania. Uwezo wetu wa nyuklia uko katika akili za wanasayansi wetu, si katika mitambo pekee.”

Amesisitiza kwamba:

“Iran haifuatilii kutengeneza silaha za nyuklia. Tunaendelea na mpango wa nyuklia kwa mujibu wa sheria za kimataifa.”

5- Msimamo wa Kidiplomasia na Ushirikiano wa Kikanda:

🔹 Iran iko tayari kwa mazungumzo ya haki na ya pande zote kufaidika na Marekani (A "win-win situation" or "win-win game").
🔹 Katika vita vya hivi karibuni, Iran imepata msaada mkubwa na wa kihistoria kutoka mataifa ya eneo, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa.
🔹 Pezeshkian amesema Iran inatafuta usalama wa pamoja wa kikanda, kwa kushirikiana na mataifa ya Kiarabu na ya Kiislamu ya jirani.

6- Kuhusu Shambulio la Qatar na Tishio la Kuuawa:

Kuhusu Shambulio la Makombora ya Iran kwenye kambi ya Al Udeid huko Qatar, Rais amesema:

“Tulilenga kambi ya Marekani iliyoshambulia Iran. Hatukuishambulia Qatar wala watu wake. Na tuliwasiliana na Amir wa Qatar siku hiyo hiyo.”

7- Kuhusu jaribio la Israel la kumuua, Rais alisema:

“Baada ya kuwaua makamanda wa kijeshi, walitaka kuwaua viongozi wa kisiasa ili kuchochea vurugu na kupindua mfumo wa Kiislamu. Hii ilikuwa sehemu ya mpango wao.”

Mwisho:
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Pezeshkian, inaonesha msimamo thabiti wa: Kujilinda, kuheshimu diplomasia, kuendeleza mpango wa nyuklia kwa mujibu wa sheria za Kimataifa, na kushirikiana na jirani zake kwa ajili ya usalama wa kweli wa kikanda - huku ikiendelea kupambana na vitisho vya wazi kutoka kwa Israel na Marekani.

Rais wa Iran ametoa Ujumbe kwa Waislamu wa Dunia nzima akisisitiza kuwa: Umoja wa Kiislamu, ujasiri, na busara ya kisiasa ndiyo njia ya kulinda heshima na usalama wa Umma wa Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha