10 Oktoba 2025 - 14:33
Msemaji wa Serikali ya Iran: Wale waliotekeleza uhalifu huko Ghaza wanapaswa kufikishwa mbele ya Mahakama

Msemaji wa serikali, huku akionyesha unga mkono kwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ghaza, alisisitiza kuwa: kusitishwa kwa uhalifu wa utawala wa Israel huko Ghaza si mwisho wa safari, na wale waliotekeleza na waliyoamuru uhalifu huu wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama za kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Fatemeh Mohajerani, msemaji wa serikali, katika mahojiano na mtandao wa Al-Mayadeen, alisisitiza kuwa Iran inatoa unga mkono kamili kwa kila mpango na hatua zitakazoweza kusababisha kusitishwa mara moja kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza. Aliongeza:

“Iran itasaidia mipango inayojumuisha kuondoka kwa majeshi ya wavamizi, kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu, kuachiliwa kwa wafungwa wa Palestina, na utekelezaji wa haki zao za msingi.”

Alisisitiza kuwa unga mkono wa Iran kwa taifa la Palestina si msimamo wa kisiasa tu, bali unatokana na imani ya kina katika haki ya mataifa ya kuamua hatima yao na kusimama imara dhidi ya ukatili na ukoloni.

Mohajerani aliashiria kuwa upinzani wa taifa la Palestina ni halali na ni sehemu ya njia ya kudumu ya kurudisha haki zao, na aliitaka jamii ya kimataifa kuchukua wajibu wake wa kisheria na kibinadamu kuhusu uhalifu wa vita na mauaji ya kimbari huko Ghaza, na kuchukua hatua kwa uthabiti kufikisha mbele ya mahakama wale waliotekeleza uhalifu huu.

Msemaji wa serikali ya Iran aliwahimiza pande zote kuwa makini na kuonya kuwa hakuna haja ya kudanganywa na utawala wa Kizayuni, na kutoruhusu kwepuka kushughulikia uvunjaji wa mara kwa mara wa makubaliano na ahadi za kimataifa.

Kauli hii ilitolewa wakati ambapo mapema alfajiri (Alhamisi), harakati ya Hamas ilitangaza kufikiwa kwa makubaliano kamili ya kumaliza vita huko Ghaza, makubaliano ambayo yamejumuisha kuondoka kwa majeshi ya wavamizi, kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu, na kubadilishana wafungwa, na kuonekana kama muhimu katika mchakato wa mabadiliko ya kisiasa ya kikanda. Makubaliano haya yalitekelezwa masaa machache baadaye.

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya kamati za Palestina na Israel kuhusiana na kusitisha mapigano huko Ghaza na kuandaa hali za kiwanja kwa kubadilishana wafungwa yalianza Jumatatu, 6 Oktoba 2025 katika Sharm el-Sheikh, Misri, na wajumbe kutoka Marekani, ikiwemo Steve Witkoff, mjumbe maalumu wa Marekani Mashariki ya Kati, na Jared Kushner, jamaa wa Donald Trump, walijiunga na mazungumzo haya.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha