Msemaji wa serikali, huku akionyesha unga mkono kwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ghaza, alisisitiza kuwa: kusitishwa kwa uhalifu wa utawala wa Israel huko Ghaza si mwisho wa safari, na wale waliotekeleza na waliyoamuru uhalifu huu wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama za kimataifa.
Sambamba na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Harakati ya Mapambano ya Kipalestina (Muqawama) na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza, vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti tetesi na tafsiri tofauti kuhusu masharti ya makubaliano hayo na namna yatakavyotekelezwa.
"Tel Aviv imelipa gharama kubwa mno katika damu ya wakaazi (walowezi wa kizayuni) wa maeneo ya Israel (bali ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel) katika vita na Iran".