8 Julai 2025 - 15:52
Mafanikio mawili ya Yemen ndani ya siku moja; Mashambulizi ya Kimaonyesho dhidi ya Hodeidah yazimwa na kushindwa/Meli "Magic Seas" Yazamishwa Baharini

Yemen, imefanikiwa kuitwanga meli iliyokuwa ikielekea maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa Kizayuni, na kuizamisha baharini.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mbali na nguvu za kijeshi na kiintelijensia za Jeshi la Ansarullah wa Yemen, uungwaji mkono mkubwa wa wananchi kwa serikali ya Yemen na Ansarullah, ni nguvu nyingine kubwa katika vita dhidi ya utawala Haram wa Kizayuni. Abdul-Malik Badr al-Din al-Houthi, Kiongozi wa Ansarullah nchini Yemen, katika mojawapo ya hotuba zake, akisifu (Muqawamah) Upinzani wa watu wa Yemen alisema: "Watu wapendwa wa Yemen kila wiki katika miezi hii wanashiriki katika maandamano ya mamilioni ya watu ambayo hayajawahi kutokea, ambayo hayapo katika nchi nyingine yoyote."

Leo pia, Wanyemen walishuhudia mafanikio mawili muhimu:

Mafanikio ya Kwanza:

Kuzima mashambulizi ya kiholela ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Al-Hudaidah.

Mafanikio ya Pili:

Kuitwanga meli iliyokuwa ikielekea maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa Kizayuni, na kufanikiwa kuizamisha baharini. Brigedia Jenerali Yahya Saree, akitangaza mafanikio zaidi ya vikosi vya jeshi vya Yemen, alisema:

"Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, meli ya 'Magic Seas' baada ya kulengwa na vikosi vyetu vya jeshi, ilizama kabisa baharini. Operesheni hii ilikuwa jibu kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria na kampuni inayomiliki meli, ambayo iliingia mara kadhaa katika bandari za Palestina inayokaliwa. Katika tukio la hivi karibuni zaidi la ukiukaji huu, meli tatu za kampuni hii, licha ya maonyo ya mara kwa mara kutoka kwa jeshi letu la majini, ziliingia bandarini za maeneo yanayokaliwa wiki iliyopita."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha