baharini
-
Iran Yaionya Marekani: Ikiwa Mzingiro wa Baharini Utaendelea, Jeshi la lran Litafanya Mashambulizi Makali Zaidi Dhidi ya Meli za Kijeshi za Marekani
Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (saww) ya Iran ameionya Marekani kwamba endapo itaendelea kuzuia na kusumbua meli za Iran baharini, Jeshi la Wanajeshi la Iran litazidisha mashambulizi makali zaidi dhidi ya meli za kijeshi za Marekani katika eneo hilo.
-
Jenerali Qaani: Dira ya Palestina Kutoka Bahari hadi Mto Bado Iko Hai na Inazidi Kufikiwa
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Esmail Qaani, amesema suala la Palestina bado ni dira hai na isiyobadilika, akisisitiza kuwa ndoto ya Palestina kutoka baharini hadi mto iko hai zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
-
Atlantic: Trump Aelekea Katika Sera ya “Kusubiri na Kuona” Dhidi ya Iran
The Atlantic inaeleza kuwa Trump sasa anaegemea zaidi mkakati wa “kusubiri na kuona”, akitumia shinikizo la kiuchumi na baharini badala ya kuongeza hatua za kijeshi dhidi ya Iran.
-
Vyombo vya Habari vya Magharibi na Israel Vyakiri Kushindwa kwa Mpango wa Muungano wa Kijeshi wa Baharini wa Saudi Arabia
Vyombo vya habari vya Magharibi na Israel vimeripoti kuwa mpango wa Saudi Arabia wa kuunda muungano wa kijeshi wa baharini katika Bahari Nyekundu umekumbana na vikwazo vikubwa, huku ukitajwa kuwa hauna uwezo wa kubadili hali ya usalama katika eneo hilo.
-
Jeshi la Yemen Latangaza Kuzuia Usafiri wa Baharini wa Saudi Arabia kwa Mujibu wa Kanuni ya “Kuzingira kwa Kuzingira”
Jeshi la Yemen limetangaza kuanza kutekeleza marufuku ya usafiri wa baharini kwa Saudi Arabia, likisema hatua hiyo ni utekelezaji wa kanuni ya “kuzingira kwa kuzingira” na kwamba liko tayari kukabiliana na aina zote za ongezeko la mashambulizi.
-
IRGC Yathibitisha kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini na anga nchini Oman
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini katika Miamba ya Salamah na rada ya udhibiti wa anga katika eneo la Ghanam nchini Oman, katika mwendelezo wa operesheni iliyopewa jina la "Nasr 2 / Ushindi 2".
-
IRGC yadai kulenga Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan kwa makombora na ndege zisizo na rubani
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), vikosi vyake vimedai kulenga majukwaa ya makombora, maghala ya mafuta na maeneo ya kuhifadhia silaha katika Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan, katika kile ilichokieleza kuwa ni hatua ya kujibu ukiukaji uliofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
IRGC yatangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz baada ya tukio la meli kupuuza maonyo
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz, likisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kile lilichodai kuwa ni ukiukaji wa maelekezo ya usalama wa baharini na kuendelea kwa uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika eneo hilo.
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Mlango wa Hormuz Hausimamiwi na CENTCOM
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kimataifa na kisheria, Kazem Gharibabadi, amesema hadhi na usimamizi wa Mlango wa Hormuz hauamuliwi na Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM), akisisitiza kuwa usalama wa eneo hilo unategemea kuheshimiwa kwa mamlaka ya mataifa ya kanda.
-
Iran yasema vikwazo vya baharini vya Marekani vimeondolewa katika bandari zake
Iran yatangaza kuondolewa kwa vikwazo vya baharini vya Marekani katika bandari zake, hatua inayoweza kufungua ukurasa mpya wa usafirishaji na biashara kati ya mataifa hayo mawili.
-
Iran: Kuachiliwa kwa Fedha Zilizozuiwa, Kuondoka kwa Majeshi ya Kigeni Mashariki ya Kati na Kulipa Ushuru wa Hormuz ni Miongoni mwa Masharti ya Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuachiliwa kwa fedha za Iran zilizozuiwa ni sehemu muhimu ya makubaliano yoyote yajayo, huku akisisitiza kuwa mazungumzo ya sasa yanajikita katika kumaliza vita na masuala ya Lebanon, na kwamba uwepo wa majeshi ya kigeni katika eneo unapaswa kukomeshwa.
-
Iran: Mashambulizi ya Marekani Dhidi ya Meli za Kibiashara Ni Tishio kwa Usafiri wa Baharini wa Kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Marekani dhidi ya meli za kibiashara za India yanatishia usalama wa usafiri wa baharini wa kimataifa na kuyataja kuwa ni mfano wa uharamia wa baharini.
-
Qaani: Kuanzia Hormuz hadi Bab al-Mandab kutaundwa “ukanda mpya wa kiusalama wa Muqawama”
Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ismail Qaani, amesema kuwa hatua za wakati muafaka na za “busara” zinazochukuliwa na Yemen zinaonyesha uimara na mshikamano wa mhimili wa Muqawama. Amesema pia kuwa, endapo kutahitajika, pande nyingine zinaweza kujiunga katika hatua hizo.
-
Gharibabadi: Haki ya Mamlaka juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz ni ya Iran na Oman Pekee
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema kuwa Iran na Oman ndizo pekee zenye haki ya mamlaka juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa hakuna nchi nyingine inayopaswa kuingilia usimamizi wa njia hiyo muhimu ya baharini.
-
Radiamali za Kimataifa kuhusu nia ya Trump kuunganisha Greenland na Marekani; Ikulu ya White House:Umuhimu wa kimkakati wa kisiwa kwa usalama wa taifa
"serikali ya Marekani kwa sasa inachunguza chaguzi mbalimbali ili kufanikisha lengo hili la kimkakati, na ikiwezekana hata “kutumia jeshi” ni miongoni mwa uwezekano unaozingatiwa na Ikulu ya White House".
-
Habari za Hivi Punde | Iran Yakamata Meli Iliyokuwa Inasafirisha Lita Milioni 4 za Mafuta ya Magendo katika Ghuba ya Uajemi
Maafisa wa Iran wamesisitiza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za kupambana na magendo ya rasilimali za taifa, kulinda uchumi wa nchi, na kudumisha usalama wa majini katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Iran Yatuma Makundi Mawili ya Kijeshi Baharini Kulinda Meli Zake
Wachambuzi wa kimataifa wanasema kuwa hatua hii inaongeza mvutano kati ya Tehran na Washington, huku ikionyesha hatari zinazoongezeka kwa usalama wa usafirishaji wa baharini.
-
Dai la Wall Street Journal: Vikosi vya Marekani Vavamia Meli Iliyokuwa Ikisafirisha Shehena ya China Kwenda Iran
Kwa mujibu wa madai ya gazeti la Wall Street Journal, vikosi maalum vya Marekani vilivamia na kuteka meli iliyokuwa ikibeba shewena ya kijeshi kutoka China kuelekea Iran katika Bahari ya Hindi mnamo Novemba 2025.
-
Trump: Hivi karibuni tutaanzisha operesheni ya kijeshi ya ardhini nchini Venezuela
Rais wa Marekani ametangaza kuongezwa kwa mashambulizi kutoka baharini hadi ndani ya ardhi ya Venezuela, na kusema kuwa Washington “hivi karibuni sana” italenga njia za ardhini zinazotumiwa kwa magendo.