13 Desemba 2025 - 13:02
Dai la Wall Street Journal: Vikosi vya Marekani Vavamia Meli Iliyokuwa Ikisafirisha Shehena ya China Kwenda Iran

Kwa mujibu wa madai ya gazeti la Wall Street Journal, vikosi maalum vya Marekani vilivamia na kuteka meli iliyokuwa ikibeba shewena ya kijeshi kutoka China kuelekea Iran katika Bahari ya Hindi mnamo Novemba 2025.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- limeripoti kuwa Wall Street Journal, likinukuu maafisa wa Marekani, limesema kuwa vikosi maalum vya Marekani vilivamia meli hiyo katika Bahari ya Hindi na kukamata shehena ya kijeshi iliyokuwa ikielekea Iran kutoka China.

Afisa mmoja wa Marekani alisema kuwa shehena hiyo ilikuwa na vipuri vyenye matumizi ya pande mbili (dual-use), ambavyo vinaweza kutumika katika silaha za kawaida za Iran. Afisa mwingine aliongeza kuwa taarifa za kiintelijensia zilizokusanywa zinaonyesha kuwa shehena hiyo ilikuwa ikielekezwa kwa makampuni ya Iran yanayohusika na usambazaji wa vipuri kwa mpango wa makombora wa Iran.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, vikosi vya Marekani vilivamia meli hiyo mamia ya maili kutoka pwani za Sri Lanka, kisha vikakamata na kuharibu shehena hiyo, na baadaye kuruhusu meli kuendelea na safari yake.

Mnamo Julai 2025 (Tir 1404), Ubalozi wa China nchini Israel ulikanusha ripoti za vyombo vya habari kuhusu madai ya China kuipatia Iran mfumo wa ulinzi wa anga, na kusisitiza kuwa Beijing haisafirishi silaha kwa nchi zinazohusika katika migogoro ya kivita.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha