Maadhimisho hayo yamefanyika mara baada ya Sala ya Ijumaa, ambapo waumini walijumuika kwa pamoja katika hali ya furaha na mshikamano, wakikata na kugawa keki mahsusi iliyoandaliwa kwa heshima ya mnasaba huo wenye baraka.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Waumini wa mji wa Nakuru, Kenya, leo wameungana katika Masjid ya Nakuru kuadhimisha tukio tukufu la kuzaliwa kwa Bibi Fatima Zahra (a.s), binti mpenzi wa Mtume Muhammad (saww), mke wa Amirul Muuminin Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na mama wa Maimamu watoharifu Imam Hassan na Imam Hussein (a.s).
Maadhimisho hayo yamefanyika mara baada ya Sala ya Ijumaa, ambapo waumini walijumuika kwa pamoja katika hali ya furaha na mshikamano, wakikata na kugawa keki mahsusi iliyoandaliwa kwa heshima ya mnasaba huo wenye baraka.
Katika hafla hiyo, Masheikh na wazee wa jamii wametoa nasaha fupi kuhusu nafasi adhimu ya Bibi Fatima (a.s) katika Uislamu, wakisisitiza umuhimu wa kuiga tabia zake za uchamungu, unyenyekevu, ukarimu na ucha-Mungu katika maisha ya kila siku.
Waumini waliohudhuria wameeleza kufurahishwa kwao na maadhimisho hayo, wakisema ni wakati wa kutafakari upendo wa Ahlul-Bayt (a.s) na kuimarisha umoja katika jamii.
Maadhimisho haya yamehitimishwa kwa du’a maalumu ya kuomba amani, baraka na mwongozo kwa waumini wote pamoja na ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Your Comment