28 Julai 2025 - 16:00
Jeshi la Yemen Latangaza Awamu ya Nne ya Kufunga Njia za Baharini, Latoa Onyo kwa Ndege Zinazosaidia Israel

Ndege yoyote, iwe ya kijeshi au kibiashara, itakayojihusisha na shughuli za kusaidia Israel, tutaiangamiza. Itaingia kwenye historia.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Julai 28, 2025 Jeshi la Yemen limetangaza rasmi kuanza kwa awamu ya nne (4) ya kampeni yake ya kijeshi ya kuzuia shughuli za baharini na angani, ikiwa ni sehemu ya kulalamikia kile walichokiita "Mashambulizi endelevu ya Israel dhidi ya Gaza" yanayoungwa mkono na Marekani.

Katika taarifa iliyorushwa kupitia vyombo vya habari vinavyohusishwa na jeshi, viongozi wa kijeshi walisema kuwa njia zote za usafiri wa baharini zenye uhusiano na maslahi ya Israel - moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja - zitaendelea kulengwa na kufungwa kikamilifu.

“Tunaingia sasa kwenye awamu ya nne ya kufunga njia za baharini. Bahari haitakuwa salama kwa yeyote anayesaidia au kusambaza bidhaa kwa utawala wa Kizayuni,” alisema msemaji mmoja wa ngazi ya juu wa jeshi hilo.

Jeshi la Yemen Latangaza Awamu ya Nne ya Kufunga Njia za Baharini, Latoa Onyo kwa Ndege Zinazosaidia Israel

Katika onyo kali zaidi, msemaji huyo alisisitiza kuwa ndege yoyote inayoshiriki au kushirikiana na shughuli zozote za Israel - iwe ya kijeshi, mizigo au kijasusi - itaangaliwa kama lengo halali la kushambuliwa.

"Ndege yoyote, iwe ya kijeshi au kibiashara, itakayojihusisha na shughuli za kusaidia Israel, tutaiangamiza. Itaingia kwenye historia".

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha