22 Julai 2025 - 15:10
Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Jeshi linasisitiza ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola katika kukomesha biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya nchini.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Wanamaji katika Operesheni zake za Kukamata Dawa za Kulevya katika Bahari ya Hindi, Mawe Mawili - Kijiji cha Kwale, Wilaya ya Mkinga - Tanga, Leo Usiku wa tarehe: 22 Julai, 2025 limefanikiwa kukamata Shehena ya Mirungi kutoka Kenya.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Ufafanuzi zaidi tukio hilo:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limekamata boti aina ya fibre, rangi nyeupe, iliyokuwa ikisafirisha mirungi kutoka Kenya kupitia Bahari ya Hindi.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Operesheni hiyo ya mafanikio ilifanyika kwa msaada wa taarifa za kiupelelezi na ufuatiliaji wa kina.

Boti hiyo ilinaswa katika eneo la Mawe Mawili, mpakani mwa Mkinga na Jiji la Tanga.

Watuhumiwa wawili waliokuwa ndani ya boti walifanikiwa kutoroka walipokaribia fukwe.

Boti na shehena ya mirungi vilikamatwa salama.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Hatua Zaidi za Jeshi la Polisi:

Jeshi la Polisi limeahidi kuimarisha doria na operesheni maalum, hasa maeneo ya Baharini yanayotumika kusafirisha bidhaa haramu.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa mapema juu ya uhalifu na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Jeshi linasisitiza ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola katika kukomesha biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya nchini.

Shehena ya Mirungi kutoka Kenya Yanaswa Baharini na Polisi Tanga Katika Msako Maalum

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha