20 Aprili 2025 - 21:01
Maandamano ya “Gaza” Islamabad: Hafidh Naeem atoa wito wa mgomo wa kitaifa na kususia bidhaa za Israel

“Tunaiheshimu nchi yetu, lakini tunataka kuwastua watawala ili wasimame na watu wa Palestina na Kashmir. Ummah wa Kiislamu umelala usingizi wa kutojali.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Islamabad: Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, Hafidh Naeem ur-Rehman, siku ya Jumapili alihutubia maandamano makubwa ya “Gaza March” yaliyofanyika mjini Islamabad, ambapo alitangaza mgomo wa kitaifa tarehe 26 Aprili ili kuonesha mshikamano na watu wa Palestina. Aliuelezea mgomo huo kama "jihad ya amani".

Akiwahutubia waandamanaji alisema: “Hatuna nia ya kugombana na yeyote, wala hatutaki mzozo na polisi, lakini hakuna mtu anayeweza kutuzuia.”

Awali, maandamano yalipangwa kufanyika mbele ya ubalozi wa Marekani katika eneo la red zone la Islamabad, lakini baada ya serikali kufunga barabara zote zinazoelekea eneo hilo kwa kuweka makontena, chama hicho kilihamishia maandamano kwenye barabara kuu ya Expressway.

Maandamano ya “Gaza” Islamabad: Hafidh Naeem atoa wito wa mgomo wa kitaifa na kususia bidhaa za Israel

Kukosoa viongozi wa Kiislamu: Hafidh Naeem alikosoa vikali ukimya wa viongozi wa Kiislamu na kusema: “Tunaiheshimu nchi yetu, lakini tunataka kuwastua watawala ili wasimame na watu wa Palestina na Kashmir. Ummah wa Kiislamu umelala usingizi wa kutojali.”

Aliongeza kuwa: “Kesi ya Palestina si ya kisiasa tu, bali ni suala la kiimani, kihistoria na kifikra. Wakati Pakistan ilipoanzishwa, harakati ya ukombozi wa Palestina nayo ilikuwa ikiendelea.”

Kukosoa Marekani na Israel: Hafidh Naeem alimuita Marekani kuwa "haitegemeki" na alisema: “Marekani si rafiki wa kweli wala adui wa kweli kwa yeyote. Hata ndani mwao, watu wanaandamana dhidi ya serikali yao.”

Alieleza kuwa maandamano dhidi ya Israel yanaendelea kote duniani: “Nchini Ulaya, Paris, Edinburgh na miji mingine mingi, watu wanaandamana kulaani uhalifu wa Israel.”

Wito kwa Umma: Katika hitimisho la hotuba yake, Hafidh Naeem aliwaambia wananchi wa Pakistan: “Ninawaomba watu wote wa Punjab, Sindh, Balochistan, Khyber Pakhtunkhwa na Gilgit-Baltistan wakusanyike chini ya bendera moja. Tuungane kama Waislamu, tuachane na mifarakano, na tufanikishe mgomo wa tarehe 26 Aprili kwa mafanikio makubwa.”

Pia alisisitiza kuhusu kuendelea kususia bidhaa za Israel na washirika wake, akisema:“Ususiaji huu si wa kiuchumi pekee, bali ni mapambano dhidi ya dhulma na ni njia ya kuunga mkono haki.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha